Sunday, June 1, 2014

YALIYOJIRI MKUTANO WA YANGA LEO---WANACHAMA WAMNGANGANIA MANJI AENDELEE KUWAONGOZA KWA MIAKA NANE IJAYO,MWENYEWE AGOMA ASEMA WAMWACHE KWANZA ATAWAJIBU



Timu  yanga leo imefanya mkutano wake wanachama katika ukumbi wa bwalo la polisi jijini dar es salaam ambapo katika mkutano huo mwenyekiti wa timu hiyo YUSUPH MANJI ametangaza kutogombea tena uongozi wa timu hiyo jambo ambalo limepingwa na wanachama wote waliokuwa katika mkutano huo,huku wakimuomba aendelee kuiongoza timu hiyo kwa miaka nane ijayo.


Wakizungumza katika mkutano huo baadhi ya wanachama wa wa timu hiyo akiwemo mke wa raisi wa zamani wa zanzibar mama karume na mzee akilimali wamesema kuwa uongozi wa manji kwenye club hiyo ni wa mfano tangu timu hiyo ianze jambo ambalo wamemtaka kuendelea zaidi ili kuisaidia timu hiyo


Mwenyekiti wa yanga akizungumza katika mkutano huo ameonekana kutoridhika na maamuzi hayo ya wanachama na kuamua kusogeza uchaguzi wa yanga mwakani ili ajipange aone kama atagombea tena.

No comments: