NI Mungu tu ambaye ataweza kuokoa mchakato wa Upatikanaji Katiba Mpya,kutokana na watu mashuhuri kushidwa kutafuta mwahafaka kwa wajumbe wanaunda Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA,mchakato huo ambao umebomolewa na Chama cha Mapinduzi CCM kuyapuuza maoni ya wananchi,
Naye,Tundu Lissu amezidi kupigilia msumari na kusema ni Ndoto kwa Wajumbe wanaunda Umoja wa katiba ya Wananchi UKAWA,kurejea kwenye Vikao hivyo vya Bunge la katiba ,kutokana na hujuma iliyofanywa Chama cha Mapinduzi kwenye mchakato huo wa Katiba.
Kauli hiyo yakukosesha Matumaini kwa watanzania,ameitoa Tundu Lissu, leo wakati alipokuwa akifanyiwa mahojiano na Mwandishi wa Mtando huu,ambapo amesema Umoja huo hautakuwa tayari kuungana katika kuwafanyia hujuma wananchi, endapo wao kurudi bungeni na kama wako watu wanaozani kama watarudi Bungeni wajue ni Ndoto ,
Maneno hayo ya Tundu Lissu ameyatoa huku ikiwa ni siku moja kupita Baada ya Jukwaa la katiba nchini (JUKATA) kumtaka Rais Jakaya Kikwete alivunje bunge hilo la Katiba.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Kaimu Mwenyekiti wa Jukata, Hebron Mwakagenda alisema kuwa bila UKAWA, Bunge hilo litakuwa feki.
Mwakagenda alisema kuwa Jukata imependekeza pia uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu uahirishwe hadi Oktoba 2015 na usimamiwe na Tume ya Uchaguzi (NEC) kwa kutumia daftari la wapiga kura litakaloandaliwa mwaka huu na kulihakiki mwakani.
Alisema kuwa wanataka Bunge Maalum la Katiba katika mkutano wake ujao kufupishwa kutoka siku 60 alizowaongeza Rais Kikwete na kubaki wiki mbili.
“Zibaki wiki mbili ili wafanye kazi moja tu muhimu ya kujadili, kuridhia na kupendekeza ratiba mpya ya mchakato wa katiba Tanzania Agosti 5 hadi 15 mwaka huu, halafu Agosti 16 liahirishwe rasmi hadi baada ya uchaguzi mkuu.
“Tunachopendekeza pia Bunge la Jamhuri ya Muungano likutane Novemba mwaka huu, kupokea rasmi hoja ya pendekezo la kuahirisha mchakato wa katiba na kupokea muswada wa marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba,” alisema.
Naye,Tundu Lissu,ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) aliumbia mtandao huu,kwa sasa hakuna nia yeyote iliyotumika katika kuokoa mchakato huo wa katiba ambao umetumia mabilioni mengi ya Wananchi.
“Nakwambia itakuwa ni Ndoto kwa UKAWA kurudi bungeni,kwani hatuwezi kuungana na CCM,kuwahujumu wananchi tukayeteketeza maoni yao,kwasababu wao CCM,wanang”angania sisi turudi halafu baadae watumisheria za Ajabu kutudanganya,na sisi hatutarudi kama mtu kati yetu anaetaka kurudi arudi tu,lakini sisi hatutokubali”alisema Lissu.
Mwandishi wa Mtandao huu alipomtaka atose Sababuza wao juzi za wao kususia Kikao cha kutafuta Suluhu,kilichoandaliwa Spika wa bunge hilo la Katiba Samwel Sitta,
Lissu,ambaye ni Mwanasheria wa CHADEMA,alisema wao walisusia Kikao hicho kwa madai ya Vikao hivyo ambavyo havina nia ya kutafuta suluhu viko kwa ajili ya kuwaomba wao warudi Bungeni na kuacha kujadili sababu ya wao kutoka kwenye Bunge hilo.
“Sikiliza Mwandishi,nakwambia huko kwenye hivyo vikao hakuna kinachojadiliwa zaidi ya kupoteza mda tu,ndio maana sisi katika kikao hiko cha pili tukaona tusitokee,kwasababu kikao cha kwanza baina yetu UKAWA,pamoja na Msajili wa Vyama vya Kisiasa nchini Francis Mutungu ilishindikana kutokana wao kupuuzia hoja zetu zilizotufanya kususia vikao hivyo”alizidi kusema Lissu.
Mchakato huo wa Katiba ambao ulifanyiwa Hujuma na Rais jakaya Kikwete wakati wa kufungua Bunge hilo la katiba,ambao alionekana kuwasaliti watanzania ambao walitoa maoni kwenye Rasimu ya pili ya katiba ,ambaye yeye na chama chake walipinga kwa nguvu zote kwa Madai ya kwamba Rasimu hiyo imehujumu maoni ya Wananchi.
Sitta awakimbia waandishi wa Habari
Katika hatua ambayo si ya kawaida, waandishi wa habari jana walisoteshwa na Ofisi ya Bunge wakati wakifuatilia taarifa hiyo ambayo awali ilikuwa itolewe juzi jioni kisha ikaahirishwa hadi jana saa 3:00 asubuhi ambapo ilielezwa kuwa Sitta angezungumza.
Hata hivyo, baada ya waandishi kufika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam, walielezwa kuwa mkutano huo haupo, lakini walipompigia simu Katibu wa Bunge aliwataka wafike Ukumbi wa Karimjee uliopo mita chache kutoka Ofisi za Bunge, saa 5:00 bila kukosa.
Walipofika katika ukumbi huo, katibu huyo hakutokea na alipopigiwa simu tena, aliwaomba waandishi waondoke na kuwataka warudi saa 7:00 mchana.
Ulipotimu muda huo, waandishi walirejea ukumbini hapo, ndipo saa 7:15, katibu huyo alitokea na kuwaelekeza waandishi warudi ofisi ndogo za Bunge, akisitiza kuwa; “Nyie nendeni mimi nitawapigia simu pale kwa kuwaomba muingie, kanisubirini nitakuja na taarifa kwani mwenyekiti anaweza asiwepo.”
Saa 8:20 mchana, katibu alifika na taarifa hiyo aliyoisoma kwa waandishi akisema kuwa Sitta alishindwa kufika kutokana na kuingiliana kwa majukumu huku akiweka angalizo kwamba hakuna haja ya kuuliza maswali kwani hakuiandaa yeye.
Endapo mchakato huo ukihalipika kama inavyonekana sasa,basi Rais Jakaya Kikwete ataingia kwenye shutuma na Lawama nzito ambazo zitamchafua hata kwenye Medani za Kimataifa,kutokana na mchakato huo kugalimu pesa nyingi za walipa kodi,
Mchakato huo,ambao ulipoteza mwelekea baada ya Kauli aliyoitoa Rais Kikwete ambaye alilenga kuyapuuza maoni ya wananchi,.
Ndipo,umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA,ambao ni muunganiko wa vyama mbalimbali ya Kisiasa ikiwemo,Chadema,Cuf,pamoja na baadhi ya wajumbe 201 kususia vikao hivyo.
No comments:
Post a Comment