
Na Karoli Vinsent.
SIKU moja kupita baada Waziri wa
Maliasili na utalii ,Lazaro Nyalandu kuifutia Leseni ya Uwindaji Kampuni Green
Miles Safari Limited(GMS) kutokana na
kuendeleza vitendo vya kutesa wanyama
pamoja na kuvunja sheria za Uwindaji,
Naye,Waziri Kivuli wa Maliasili na
Utalii,Mchungaji Peter Msigwa,ameibuka na kumtaka Waziri Nyalandu kupitia Upya
Kampuni zote za Uwindaji hapa nchini kwani nazo zimekuwa zikifanya kazi kinyume
na sheria.
Kauli hiyo ya Msigwa ameitoa Mda huu
wakati alipokuwa anafanyiwa Mahojiano na Mwandishi wa Mtandao huu kwa Njia ya
Simu kutoka Iringa,ambapo Mwandishi wa Mtandao huu alitaka kujua anachukuliaje
Hatua iliyochukuliwa na Waziri nyalandu kufungia kampuni hiyo ya Uwindaji.
Ndipo, Msigwa alisema ni mda umefika kwa
Waziri Nyalandu kupita upya kampuni zinazofanya Ujangili hapa nchini kwani
zimekuwa zikifanya kazi kinyume na taratibu.
“Katika hili nampongeza kwa kuchuka
Hatua,cha msingi namtaka asiishie kwenye Kampuni hii,inabidi kuyachukulia
makumpuni mengine ya uwindaji, tena inabidi achunguze kwa makini kampuni
zengine ambazo zimekuwa zinafanya ubabaishaji kwenye uwindaji hapa
nchini”alisema Msigwa
Mchungaji Msigwa,ambaye ni Mbunge wa
Iringa Mjini CHADEMA,alimpongeza Waziri Nyalandu kwa kitendo chake cha kutoa
itikadi zake za Chama na kuweka Maslahi ya Taifa mbele kwani suala la Uwindaji
haramu linapaswa kupigwa vita na kila mtu mpenda maendeleo katika Taifa hili.
Katika Hatua nyingine
Mwandishi wa Mtandao huu alipomtaka atoe ufafanuzi kuhusu Taarifa zinazoandikwa
kwenye Magazeti mbalimbali hapa nchini .
Kwamba kitendo chake cha kupinga kampuni
hii iliyofungiwa ya Uwindaji Kampuni Green Miles Safari Limited(GMS)
inatokana na Yeye kufanya Njama ili Kampuni ya Wengbert Windrose Safari
(WWS)inayomilikiwa na Wamarekani ipewe kitalu hicho cha Uwindaji kilichipo Ziwa
Natrion?
Msigwa akijibu kwa Hasira alisema
anashindwa kuwaelewa Waandishi wa Habari wa nchi hii, kushindwa kujibu hoja ya
yeye aliyoibua kuhusu unyama huo unaofanya na Kampuni hiyo uwindaji Green Miles
Safari Limited(GMS).
“Mimi ningetegemea Mwandishi makini wa
Habari angeibuka nakupinga ushahidi ule na kujibu hoja kwamba niliyosema yana
uongo au la kwamba Wanyama wale hawapigwi,lakini kusema kwamba mimi naipendelea
kampuni hiyo sio za Kweli”
“Kwahiyo kama wao wana ugomvi na Kampuni
nyingine mimi hayanihusu,mimi hapa nazungumzia ukiukaji wa haki na kwamba kama
ipo kampuni nyingine ikifanya kinyume na taratibu mimi nakufa nayo”alisema
Msigwa.
Mwandishi wa Mtandao huu alipotaka kujua
kama hatayachukulia hatua zozote za kisheria Magazeti haya ambayo yamekuwa
yakimshutumu kwamba amehongwa na kampuni hiyo ya Wengbert Windrose Safari
(WWS)inayomilikiwa na Wamarekani ?
Mchungaji,Msigwa ambaye ni Mwanasiasa
Machachari kutoka Chadema alisema Hawezi kubishana na Watu waliokosa maana,
yeye anakazi nyingi za kufanya.
“Mwandishi kuna kazi nyingi sana za
kufanya siwezi nikabishana na watu wasiojielewa kwani mtu akiandika kama
mimi ni mwanamke harafu eti mimi nianze kubishana na mtu aliyeandika hivyo wakati
mimi ni mwanaume,mimi nawaacha waandike najua wataacha”
“Mimi kukaa na Wajinga ambao wanatumiwa
na watu binafsi ili waweze kukwamisha kasi yangu ya kulinda wanyama pori hapa
nchini”alisema Msigwa.
Mchungaji Msigwa ndiye mtu aliyeibua
hujuma inayofanywa na Kampuni uwindaji Green Miles Safari Limited(GMS) kupitia
mkanda wa Video ambapo msigwa alisema Kampuni hiyo imekuwa ikifanya uwindaji
kinyume na taratibu.
Ndipo,jitihada hizo za Mchungaji Msigwa
zilimuibua Waziri wa Maliasili,Lazaro Nyalandu,na kuifutia Leseni kampuni hiyo,
Akisoma
maazimia hayo jana mbele ya Waandishi wa Habari waziri Nyalandu alitaja makosa
hayo kuwa ni wageni wa kampuni hiyo kuwinda wanyama ambao hawakuruhusiwa kwenye
leseni ya uwindaji wakiwemo nyani na ndege, jambo ambalo ni kinyume na kifungu
cha 19(1)(2).
Pili,
wageni wa kampuni hiyo kuchezea watoto wa pundamilia na ngiri kinyume na
kifungu cha (19)(1), wageni kufukuza wanyamapori kwa magari na kisha kuwapiga
risasi wakiwa ndani ya magari kinyume na kifungu 65(1) (a) 1, kuwinda wanyama
walio chini ya umri (watoto), kinyume na kifungu cha 56(1).
“Kuruhusu
watoto chini ya miaka 16 kuwinda kinyume na kifungu cha 43(2) (a), na wageni
kuwinda huku wakipiga kelele, jambo ambalo ni kero kwa wanyama na kinyume na
kifungu cha 19(1) na (2),” alisema.
Nyalandu
alikiri kampuni hiyo kuvunja sheria ya wanyamapori ya mwaka 2009, sambamba na
kanuni za uwindaji, na kwamba kwa kuzingatia mamlaka aliyopewa chini ya sheria
hiyo ya kuhifadhi wanyamapori No.5, amechukua hatua.
“Kwa
kuzingatia matakwa ya kanuni ya 17(1), 8(2), nafuta umiliki wa vitalu vyote
vilivyo chini ya Kampuni ya Green Miles Safaris Ltd, hii ikiwa ni pamoja na
vitalu vya Lake Natron GC East, Gonabis/ Kidunda-WMA na MKI-Selous.
“Pia, hatua hii inafuta vibali vyote vya uwindaji
vilivyotolewa katika msimu huu wa uwindaji na hii iwe onyo kwa kampuni za
uwindaji wa kitalii nchini kuhusu ukiukwaji wa sheria, kanuni na taratibu za
uwindaji,” alisema
No comments:
Post a Comment