SIKU moja kupita Baada ya Gazeti la Tanzania Daima kufichua kile ilichokiita ni hujuma mbaya ya Kisiasa anayoifanya Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CCM) kwa kushirikiana na wanachama waliofukuzwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kwa usaliti kwenye chama hicho.
Wanachama hao ambao wamejiunga na Chama kipya cha kisiasa cha Allaince for Change and Transparency (ACT-Tanzania) chama ambacho inasemekana kinaubia na Chama kikuu nchini kwa lengo la kukiboma Chadema.
Naye Katibu Mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Dk Wilbroad Slaa,ameibuka na Kumvaa Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CCM na kusema Chadema hakina mda wa kupoteza na kupambana mtu mwenye Tamaa ya Urais huku akijua hana sifa kushika nafasi hiyo.
Kauli hiyo kali Imetolewa Mda huu na Katibu huyo Mkuu wa Chadema Dk Wilbroad Slaa wakati alipokuwa anaongea na Mwandishi wa Mtandao huu kwa njia ya Simu kuhusu taarifa iliyoandikwa kwenye Gazeti hilo la kila siku kuhusu mipango hiyo michafu ya kisiasa.
Ambapo alisema Taarifa hizo amezisikia na kusema chadema hakina mda mchafu wa kumfikilia mtu anayetafuta nafasi ya Urais huku akijua hana sifa.
“Ngoja nikwambie Chadema imejipanga kuhakisha tunafika mbali kisiasa na hatuna mda mchafu wa kupambana na mtu anayesaka Urais huku hakijua hana sifa, kwanza haya ni Maajabu mimi najua vyama vinazaliwa ili kupambana na chama kilichopo madarakani ambacho kimeshindwa kuondoa umasikini kwa mda wa miaka 50 nashangaa leo hiko chama cha ACT kinaungana ili kupambana na chama cha upinzani?”Alihoji Dk Slaa
Dk Slaa ambaye chama chake ndicho chama kikuu cha upinzani Nchini ambacho kinaanza kufanyiwa Hujuma, alikitabilia mwisho Mbaya chama hicho kipya cha kisiasa cha Allaince for Change and Transparency (ACT-Tanzania) na kusema kama kimeanzisha na Mamluki ili kije kupambana na Upinzania hapa nchini Basi hakitafika mbali na kufuata nyayo ya vyama vilivyokuwa huku nyuma.
Katika Hatua nyingine Dk Slaa,alisema kwa sasa wamebaini kuna Mamluki wameanza kupenyeshwa ndani ya Chadema kuelekea uchaguzi wa ndani wa chama cha CHADEMA.
“Na sahivi chadema imegundua kuna mamluki wameanza kuingizwa kwenye chaguzi zetu za ndani kwa malengo ya kutumaliza kisiasa na sisi tuko makini sana na tunawahakikishia wanachama wetu tutawaondoa Mamluki wote waliopenyezwa watu wasiokuwa na mapenzi mema ya chama chetu”Alisema Dk Slaa.
Kauli hiyo ya Katibu huyo mkuu wa Chadema baada ya Taarifa iliyoandikwa kwenye Gazeti la Tanzania Daima ambapo taarifa hiyo ilimtuhumu Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CCM) ndiye mfadhili mkuu na mpanga mikakati mkuu wa kundi linalomfuata Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), ambalo limeanzisha chama kipya cha siasa, Allaince for Change and Transparency (ACT-Tanzania).
Kwa mujibu wa vyanzo hivyo vya habari, Lowassa amejiaminisha kwamba ndiye atakayekuwa mgombea urais kupitia CCM. Kazi kubwa anayoona mbele yake ni kuanza mapema kusambaratisha CHADEMA ili kupunguza upinzani wakati wa kampeni utakapofika.
Zitto naye, ambaye uanachama wake kwa CHADEMA umebaki kwenye makaratasi tu, anatajwa kuwa ndiye mwasisi mwenza wa ACT, na amekuwa na uhusiano wa “kikazi” na Lowassa, hata kabla hajaingia kwenye matata ya wazi na chama chake, ambacho mwishoni mwa mwaka jana kilimvua vyeo vyake vyote vya uteuzi ndani ya CHADEMA kwa tuhuma mbalimbali.
Katika hatua mojawapo, chanzo kimoja kilicho karibu na Lowassa kimesema kwamba mapema mwaka juzi, Zitto alimwendea Lowassa na kumwambia kuwa mustakabali wake kisiasa ndani ya CHADEMA si mzuri, na kwamba alikuwa tayari kumsaidia Lowassa kufanikisha malengo yake, lakini kwa sharti kwamba iwapo mbunge huyo wa Monduli atafanikiwa kupata urais, basi amteue kuwa Waziri Mkuu
No comments:
Post a Comment