Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za Binadamu Bi HELLEN KIJO BISIMBA akizungumza na waaandishi wa habari mapema leo kuhusu Repoti hiyo |
Kituo
cha sheria na haki za binadamu tanzania LHRC leo kimetoa report yake ya nusu
mwaka ya haki za binadamu report ambayo inaonyesha bado hali ya haki za binadamu kwa Tanzania ni
tete na jitihada za serikali bado zinahitajika kujinasua na hali hiyo.
Katika
repoti hiyo ya miezi sita tu inaonyesha
kuwa watu 320 wameuawa kwa imani za
kishirikina ukilinganisha na watu 303 waliouawa mwaka jana pamoja na matukio 473 yameripotiwa kuuawa kwa watu na
wananchi wanaojiita wenye hasira kali ukilinganisha na matukio 597 ya mwaka
jana ambapo takwimu inaonyesha kupungua,
Mwanasheria kutoka LHRC, MLOWE akifafanua yaliyomo ndani ya Report hiyo |
Aidha report hiyo inaonyesha matukio ya mauaji ya
watu wenye ulemavu wa ngozi yameanza kuongezaka kwa kipindi cha miezi sita
iliyopita ambapo watu wawili wameripotiwa kuuawa na wengine kujeruhiwa vibaya.
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es
salaam mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho bi HELLEN KIJO BISIMBA amesema kuwa maswala
mengi kama mauaji ya vikongwe,mauaji ya walemavu wa ngozi,migogoro ya
ardhi,ajali za barabarani,wananchi kujichukulia sheria mkononi,na mambo mengine
kama hayo bado ni changamoto kubwa kwa nchi ya tanzania ambapo amesema ni
lazima serikali akazie mkazo maswala hayo.
Wanahabari wakisikiliza kwa makini |
Bi HELLEN amesema kuwa ili kudhibiti hali hii ni
lazima kwa elimu ya haki za binadamu irudishwe kwenye mfumo wa elimu rasmi wanchi,pamoja
na serikali kutunga sheria inayolinda haki za mtoa taarifa ili kuweza kupata
ushirikiano wa wananchi katika mapano dhidi ya vitendo viovu.
Aidha ameitaka serikali kuboresha mifumo ya utoaji
haki ikiwa ni pamoja na mahakama na mabaraza mbalimbali ya utatuzi wa migogoro
ili kukuza dhana ya utawala wa kisheria nchini
Report hiyo imetoka leo ikiwa ni siku ya maadhimisho
ya siku ya wanawake wa Africa inayoadhimishwa kote Africa.
No comments:
Post a Comment