JESHI la polisi Tanzania limetoa wito kwa wananchi kutojihusisha na mikusanyiko isiyokuwa ya lazima ikiwa ni pamoja na kuwa makini na mtu ama kitu chochote watakachokitilia shaka pamoja na kuendelea kutoa taarifa ili kuwabaini wahalifu wote wanaojihisisha na milipuko ya mabomu ambayo imeendelea kutokea kwa kasi hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kamishna wa polisi ISAYA MNGULU kuhusu mlipuko wa bomu uliotokea jana mkoani arusha katika mgahawa wa VAMA TRADITIONALY INDIAN CASINO jirani na viwanja vya gimkana mlipuko ambao umesababisha madhara ya majeruhi zaidi ya watu nane amesema kuwa jeshi la polisi linaendelea na upelelezi wa tukio hilo pamoja na matukio mengine kama hayo ili kuwabaini wale wote wanaohusika na milipuko hiyo huku akuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo.
MNGULU amesema kuwa katika matukio mengine ya nyuma jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata jumla ya watu 20 wakiwemo watu sita wanaosadikiwa kujihusisha na mlipuko wa bimu uliotokea tarehe 3,mwezi wa saba nyumbani kwa sheik SUDU ALLY mkoani arusha.
Matukio ya milipuko ya mabomu kwa sasa yamekuwa yakiripotiwa kwa kasi sana katika mkoa wa arusha na Zanzibar ambapo hadi sasa bado jeshi la polisi halijapata chanzo halisi cha milipuko hiyo pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa na jeshi hilo.
No comments:
Post a Comment