Thursday, August 7, 2014

HABARI KUBWA LEO--CCM YAWACHARUKIA WAJUMBE WA TUME YA WARIOBA,NAPE AWAPA ONYO KALI,SOMA HAPA

Na Karoli Vinsent

 CHAMA cha Mapinduzi CCM kimewataka wajumbe wa iliyokuwa Tume ya ukusanyaji wa Maoni ya Katiba kuachama mara moja Tabia ya kufanya mchakato wa katiba mpya ni mali yao kwani wao hawana Mamlaka hiyo kisheria.

        Kauli hiyo Imetolewa leo na Katibu wa Halmashauri kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi wa chama cha Mapinduzi CCM,Nape Moses Nnauye wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari ofisi ndogo za Chama hicho jijini Dar Es Salaam,ambapo alisema Baadhi ya wajumbe wa Tume ya Warioba wameufanya mchakato wa katiba kuwa mali yao binafsi.


        Kauli hiyo ya Nape inatokana Mdahalo ulioandaliwa hivi karibuni na Taasisi ya Mwalimu Nyerere ambao mdahalo huo uliwashirikisha wajumbe mbalimbali wa tume ya warioba pamoja na mwenyekiti wa tume hiyo ambaye n iJaji Warioba mwenyewe,

         Ambapo Nape alisema wajumbe hao katika mdahalo huo walionekana wazi kumbeza Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM Rais Jakaya Kikwete,kwa kusema yeye ndiye aneuhujumu mchakato huo wa katiba mpya.

      “Mara Kadhaa na hata katika mdahalo huo,baadhi ya waliokuwa wajumbe wa Tume ya Warioba waekuwa wakitumia muda mwingi kujaribu kupotosha Umma na kuwashambulia wenye mitazamo tofauti nay a kwao”

      “Kudhihilisha ukweli huo,sasa wazee hao wameonesha hasira zao kwa kutumia kauli za Dharau na Kejeli kwa Rais ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa,na wamekuwa wakitumia lusha kali na hata kutumia uzee”alisema Nape.

        Aidha,Nape alisema kwa sasa chama hicho hakiwezi kuvumilia hali hiyo,na kitajibu mapigo kila itakapowezekana na kusema pia tabia ya kumzushia Rais Kikwete alivyokwenda kufungua Bunge Maalum la Katiba kwamba ndio sababu ya kubezwa ni uongo.

          “Nashangaa sana Mzee wetu warioba navyomsema vibaya Rais Kikwete kwamba alivyokwenda kuzindua Bunge la katiba ndio kosa, wakati sio kweli Rais naye ni mtanzania anapashwa kutoa maoni yake kama mtanzania mwengine lakini leo ndio imekuwa niongwa?”alihoji Nape.

         Katika hatua Nyingine Chama hicho kimewatetea Makada wa chama hicho ambao walionekana kwenda kinyume na misimamo ya chama hicho,wakiwemo Naibu Katibu Mkuu wa chama cha Mapinzuzi ccm Bara,Mwigulu Nchemba pamoja na Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe ambao walitaka Bunge hilo la katiba livunjwe kwani limekusa Maridhiono ya kisiasa kutokana na kutokuwepo upande mmoja wa Kisiasa ambao ni Ukawa.

         Badala yake chama hicho kimesema hayo ni Maoni ya mtu yanapashwa kuheshimiwa na chama hicho hakina ugomvi na makada wake wowote wanapofikia hatua ya kutoa maoni.

        Wakati huohuo Chama hicho kimesema hakiwezi kutishwa na hatua ya waliyoifanya Umoja wa kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA kususia na kushindwa kurejea kwenye Bunge maalum la katiba na kusema hata wasiporejea katiba itapatikana tu kwani hao ukawa ni watu wachache sana hawawezi kukwamisha mchakato huo.
  
           “Nataka niwambie watanzania kwamba katiba mpya itapatika hata bila kuwepo hao wanaojiita Ukawa,kwani ukingalia hiyo hoja wanayosema kwamba 2 ya 3 yawajumbe itapatikana na ukiangalia wajumbe wabunge hilo wanazidi idadi hiyo kwanini sasa tuwaogope watu wachache wasiokuwa na hoja ,nawahakikishia katiba Mpya itapatikana tu”alisema Nape

No comments: