KATIKA kukabiliana na tatizo la Msongamano wa Magari Mkoani Dar es Salaam,Serikali imesema iko mbioni kujenga Reli kutoka Ubungo jijini hapa hadi Bagamoyo Mkoani pwani ili kupunguza tatizo hilo kubwa linalowakabili watanzania kwa sasa.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi
Kutokana na serikali kupanga kujenga Reli kutoka Ubungo hadi Bagamoyo mkoani Pwani
“Serikali imeliona tatizo hili msongamo wa magari na sasa tumepanga kujenga Reli itakayotoka ubungo hadi Bagamoyo na reli hii itasaidia kwa kiwango kikubwa sana kuwapunguzia adha ya wananchi waliokuwa wanaipata,na tayari serikali katika Bajeti ya Fedha ya Mwaka 2014-2015 tumetenga fedha kwa ajiri ya upembuzi yakinifu katika mpango huu wa Ujenzi wa reli na tunawahakikishia watanzania mradi huu utakamilika ipasavyo”alisema Dkt Mwinjakana
Vilevile Mwinjakana alizidi kusema Baada ya uchambuzi yakinifu Serikali itaanza Rasmi ujenzi wa Reli hiyo na kusema Watanzania wategemee makubwa kutokana na ujenzi wa Reli hiyo,ambapo alisema mpango wa ujenzi wa Reli ni miongoni mwa mipango ya “Big Result now” yaani matokeo makubwa sasa.
Katika Hatua nyingine Wizara hiyo ya Uchukuzi imesema Ujenzi wa “Terminal Three” kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu Julias Nyerere utakamilika Mwakani Mwezi wa Sita na kusema Terminal hii itaweza kupokea watu milioni sita na kupelekea uwanja huo kuwemo katika viwanja vikubwa kabisa barani Afrika.
No comments:
Post a Comment