KANSA MOHAMED MBARUKU akiwa anasindikizwa na walinzi wake wakati akirudisha form yake ya kugombea uenyekiti katika ofisi za makao makuu ya chama hicho jana jioni. |
Wakati homa na joto la uchaguzi ndani ya chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA likizidi kupanda kadiri siku zinavyozidi kwenda mbele hatimaye mwanachama mwingine amejitokeza na kuchukua form ya kugombea nafasi ya mwenyekiti wa chama na kufikisha idadi ya watu wawili walioitaka nafasi hiyo huku mmoja akiwa ni mwenyekiti wa sasa na mbunge wa hai mh FREMAN MBOWE.
KANSA MOHAMED MBARUKU pichani ndiye mwanachadema aliyejitokeza jana jioni kwa ajili ya kupambana na mwenyekiti wake wa sasa FREMAN MBOWE katika nafasi ya kukiongoza chama hicho katika ngazi ya taifa yani mwenyekiti.
Akizngumza na mtandao huu baada ya kurejesha form hio MBARUKU alisema kuwa lengo la kuitaka nafasi hiyo ni kuhakikisha kuwa chama hicho kinasimama na kuondokana na kashfa mbalimbali ambazo zimekuwa zikijitokeza hususani za kibaguzi ambazo anasema zinashusha hadhi ya chama hicho.
No comments:
Post a Comment