Mkurugenzi wa uwezeshaji na uwajibikaji wa kituo hicho IMELDA URIO wakati akisoma tamko la kituo hicho kuhusu mwenendo wa mchakato wa katiba |
Ikiwa bado wadau mbalimbali nchini wakiendelea
kupiga kelele kutaka bunge maalum la katiba lisimamishwe mara moja kwa kile
wanachodai ni wizi wa fedha za watanzania ndani ya bunge hilo,nao Kituo cha
sheria na haki za Binadamu nchini LHRC
wameibuka na kumtaka na Rais wa jamhuru ya muungano wa Tanzania kuchukua hatua
mara moja ya kulisimamisha bunge hilo hadi maridhiano ya ukweli
yatakapopatikana.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na
mkurugenzi wa uwezeshaji na uwajibikaji wa kituo hicho bi IMELDA URIO wakati
akisoma tamko la kituo hicho kuhusu mwenendo wa mchakato wa katiba hadi hapa
ulipofikia,ambapo amesema kuwa wamekuwa wakifwatilia kwa ukaribu mchakato huo
na kutoa maoni yao ambayo kwa kiasi
kikubwa yamekuwayakipingwa kwa maslahi ya kisiasa.
Wanahabari wakisikiliza kwa makini |
BI EMELDA anasema kuwa kumekuwa na kauli za
kuwachanganya watanzania juu ya uwezo wa Rais kulivunja bunge hilo akitolea
mfano kauli ya mwanasheria mkuu wa serikali aliyoitoa mnamo tarehe 17 mwezi wa
nane kuwa Rais hana mamlaka ya kulivunja bunge hilo kwa madai ya kutokuwepo kwa
kipengele cha sheria ambapo amesema kuwa
kauli hiyo haina maslahi wala uchungu wa watanzania ambao ndio walipa kodi
zinazowalipa kodi wajumbe hao.
Aidha ametolea mfano kauli nyingine aliyoitoa
mwenyekiti wa bunge hilo mh SAMWELI SITTA ambapo alisikika akisema kuwa pamoja
na makubaliano ya kuahirisha bunge hilo hadi baada ya uchaguzi na kusema
upigaji kura wa kifungu kwa kifungu uko pale pale pamoja na uwezekeno wa theluth
mbili kutopatikana, huku akitaka kuwashirikisha watanzania walioko nje ya
nchi,wagonjwa na wale walioko hijja, Kituo cha sheria wamesema kuwa mwenyekiti
huyo anafanya hayo yote huku akijua wazi kuwa anapotosha umma.
Katika hatua nyingine LHRC wamesema kuwa swala la
uchaguzi halihusiani kabisa na mchakato wa katiba mchakato wa katiba unaweza
kabisa kuendelea na uchaguzi sambamba kwani rasimu ya katiba hususani ibara ya
268 inatoa kipindi cha mpito cha miaka minne kabla ya kuanza kutumia katiba
mpya.hivyo kusitisha mchakato wa katiba kwa kisingizio cha uchaguzi ni kosa
kubwa sana ambalo linatokana na kuwaachia wanasiasa mchakato huo ambapo
wamesema kuwa wanasiasa kazi yao kubwa ni kuangalia maslahi yaoya kuwepo
madarakani na si maslahi ya wananchi.
LHRC ni wadau wengine waliojitokeza kupinga mwenendo
wa bunge hilo huku kukiwa na wimbi la watu mbalimbali wakiwemo wanasiasa,asasi
za kiraia ambao nao wamekuwa wakitaka bunge hilo liahirishwe mara moja
No comments:
Post a Comment