Thursday, September 4, 2014

LIVE TOKA BAGAMOYO--WATAALAM WA MATIBABU KWA NJIA YA MTANDAO WAKUTANA LEO BAGAMOYO,WAZIRI MAKAME MBARAWA MGENI RASMI--STORY NZIMA IPO HAPA

Mgeni rasmi katika shughuli hiyo ambaye ni waziri wa mawasiliano,sayansi na technologia mh MAKAME MBARAWA akizungumza wakati akitoa Hotuba yake fupi ya ufunguzi rasmi wa mkutano huo wa siku mbili wa wataalam wa maswala ya matibabu kwa njia ya mtandao mkutano ambao unafanyika Wilayani Bagamoyo.picha na EXAUD MTEI WA HABARI24 BLOG
    Waziri wa mawasiliano sayansi na technologia mh MAKAME MBARAWA leo amezindua mkutano wa siku mbili wa wadau wa huduma ya matibabu kwa njia ya mtandao (TELEMEDICINE)  wenye lengo la kujadili jinsi ya kuboresha huduma hiyo pamoja na changamoto zake.
      
Akifungua mkutano huo waziri MBARAWA amesema kuwa huduma ya telemedicine ni muhimu sana kwa wananchhi wa Tanzania,kutokana na ukweli kuwa ni huduma ya haraka na isiyogharimu  kwenda umbali mrefu.

Huduma hiyo ambayo iliyofanyiwa  majaribio katika hospitali saba nchini imeonyesha mafanikio makubwa  na hivyo serikali inafikiria kuziunganisha  hospitali zote muhimu za wilaya na mikoa hapa nchini na huduma hiyo.
Nachangia kidogo--mtaalam
Akizungumzia jinsi huduma hiyo inavyofanya kazi waziri mbarawa amesema kuwa  ni huduma ambayo inatafutwa kama huduma nyingine isipikuwa utofauti wake ni huduma ambayo inapatikana  kwa haraka kutokana na kuhusisha mtandao.
Wdau mbalimbali wanaohudhuriaa katika mkutano huo wakiwa makini kusikiliza.
Kwa mujibu wa huduma hiyo ni kwamba Daktari  anaweza kuwasiliana  na Daktari ambaye yupo hosipitali nyingine na kuweza kutoa maelekezo moja kwa moja kwa daktarri husika  kwa ajili ya kumhdumia mgonjwa na huuduma kuendelea kama kawaida.
Huduma hiyo ambayo kwa mara ya kwanza ilizinduliwa na raisi wa Tanzania MH JAKAYA MRISHO KIKWETE mwaka 2011 na kuanza kufanya kazi mwaka 2012 imegharimu zaidi ya million 85 hadi sasa na waziri mbarawa amewataka watanzania kuiamini kwani ni mapinduzi katika secta ya afya na mtandao.

Aidha katika hatua nyingine wizaya yake pamoja na wizara ya afya wamekubaliana na mtandao wa VODACOM TANZANIA kuanza kutoa huduma ya mtandao bure katika hospitali ya taifa muhimbili ikiwa ni jitihada za kurahisisha huduma katika hospitali hiyo
Waziri MAKAME MBARAWA akiwa katika picha ya pamoja na wataalam mbalimbali mara baada ya kuzindua rasmi mkutano huo leo wilayani bagamoyo

UKITAKA KUFAHAMU JINSI HUDUMA HII INAVYOFANYA KAZI TAFADHALI BONYEZA HAPO CHINI--


 Mama yako mzazi yu mgonjwa mahututi katika hospitali ya Wilaya ya Masasi. Madaktari wamelifahamu tatizo lake lakini hakuna vifaa wala wataalamu wa jinsi ya kumtibu. Anatakiwa ahamishiwe Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako kuna madaktari bingwa na vifaatiba vya uhakika. Hata hivyo safari ya kutoka Masasi hadi Dar Es Salaam, pengine yaweza... kupoteza uhai wake.
Lakini usihofu... Tanzania sasa imepata neema baada ya kuwepo kwa huduma ya Tiba kwa njia ya Teknolojia ya habari na mawasiliano, kwa kitaalamu ‘telemedicine’ 
Telemedicine ni utoaji wa huduma za afya au mbadilishano wa taarifa za kitiba kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano.
Mafanikio ya uvumbuzi huu yamesaidia  wataalamu wa afya kubaini na kutibu wagonjwa bila kuonana nao uso kwa uso.
Kwa kifupi, unaweza ukazungumza na daktari wako na kumweleza vile unavyojisikia, kisha akakuandikia vipimo, na baada ya kumpa majibu ya vipimo hayo kwa njia ya teknolojia pia, atakuandikia dawa au kukupa ushauri wa kitiba.
 Pia, Hospitali yenye vifaa na wataalamu wanaweza kuzungumza na madaktari katika hospitali za vijijini na kutoa ushauri wa jinsi ya kumtibu mgonjwa aliye taabani. 
Hivi sasa hospitali nne nchini zimeunganishwa katika mradi  huo wa Telemedicine ambazo ni Mwananyamala, Amana, Temeke na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH) pamoja na hospitali ya Tumbi, Mkoa wa Pwani.
Mei, 2011 ndiyo wakati ambao Rais Jakaya Kikwete alizindua  mradi huu akiwa pamoja na Makamu wa Rais wa India, Dk Manmohan Singh.
Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Modou Gaye anasema teknolojia hii inawezesha madaktari walioko katika Hospitali za Amana, Mwananyamala, Temeke, Tumbi na Bagamoyo kuwasiliana moja kwa moja na madaktari bingwa pamoja na watalaamu wengine walioko Muhimbili katika kujadili, kushauriana na hatimaye kufanya uamuzi kuhusiana na tiba, uchunguzi wa mgonjwa husika.
Gaye anasema kuwa teknolojia hii itamwezesha mgonjwa aliyeko kati ya hospitali hizo kupata matibabu bila kufika Muhimbili.
Anasema kupitia teknolojia hii wataalamu wataweza kuwasiliana katika nyanja za ushauri, vipimo vya uchunguzi mathalan vya radiolojia,  vipimo vya uchunguzi vya patholojia, magonjwa ya moyo na mafunzo kwa watalaamu.
Uwepo wa teknolojia hii utawezesha mgonjwa anayehitaji kupata huduma za kibingwa Muhimbili kutibiwa haraka na kwa muda mfupi kuliko ambayo angefuata utaratibu wa rufaa na hivyo kumpunguzia muda wa kukaa hospitalini kwa muda mrefu.

No comments: