Wednesday, September 3, 2014

michezo--MECHI ZA KIMATAIFA ZA KIRAFIKI..ROONEY NA DI MARIA WATISHA USIKU HUU,TIZAMA HAPA


Nahodha babu kubwa; Wayne Rooney akipongezwa na wenzake baada ya kufunga bao pekee usiku wa leo
NAHODHA wa England, Wayne Rooney ameitendea haki beji katika mchezo wake wa kwanza tangu arithi mikoba ya Steven Gerrard aliyestaafu, baada ya kufunga bao pekee katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Norway Uwanja wa Wembley usiku huu.


Nahodha huyo wa Manchester United pia, alifunga bao hilo pekee kwa mkwaju wa penalti dakika ya 68, kufuatia nyota wa Liverpool, Raheem Sterling kuchezewa rafu kwenye eneo la penalti.

Katika mchezo huo uliohudhuriwa na watu 40,181 – idadi ndogo zaidi ya mahudhurio kwenye Uwanja wa Wembley tangu ufunguliwe tena, kinda Sterling alizawadiwa heshima ya mchezaji bora mechi baada ya kazi nzuri kwenye kikosi cha Roy Hodgson usiku wa leo

Kifaa halisi; Angel di Maria ameng'ara vilivyo leo Argentina ikilipa kisasi cha Kombe la Dunia kwa Ujerumani 


WINGA Angel di Maria ametengeneza mabao matatu na kufunga moja, Argentina ikilipa kisasi cha Kombe la Dunia kwa kuifunga 4-2 Ujerumani usiku huu katika mchezo wa kirafiki mjini Dusseldorf, Ujerumani.

Mchezaji huyo ghali zaidi kuwahi kusajiliwa Manchester United na Uingereza nzima alipika mabao ya Sergio Aguero, Erik Lamela na Federico Fernandez kabla ya kufunga na lake mwenyewe siku 52 tangu bao la Mario Gotze katika muda wa nyongeza liipe Ujerumani ubingwa wa dunia nchini Brazil.

Mabao matano kati ya sita yamefungwa na wachezaji wa Ligi Kuu ya England, huku Andre Schurrle akiifungia Ujerumani kabla ya Gotze kuwafungia bao la pili mabingwa hao wa dunia. 

No comments: