Tuesday, September 23, 2014

TAARIFA KWA UMMA KUKANUSHA UVUMI WA KUAJIRI VIJANA 500 NA KUWAPATIA MASOMO YA MAFUTA NA GESI-TPDC

SHIRIKA LA MAENDELEO YA PETROLI TANZANIA
Tanzania-Petroleum-Development-Corporation-TPDC
Kuna taarifa zimeendelea kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikiwa na maelezo kuwa: ” Serikali kupitia Shirika la Elimu Tanzania, TPDC kwa ushirikiano na kampuni za oil and gas, wanatarajia kuajiri vijana wapatao 500 katika sekta hii mpya Tanzania kuanzia mwezi Januari na Machi 2015, hivyo 
wameandaa crush program itakayoanza 6 Oktoba 2014. Walengwa ni vijana wenye elimu ya form 4 na form 6 ambao watasoma kwa miezi 6 na kupelekwa kwenye ajira  moja kwa moja baada ya kuhitimu!..kwa wale wenye elimu kuanzia diploma watasoma kwa miezi 3, kozi ya oil and gas management!…Ada kwa kundi la kwanza ni tshs 1,150,000 na kundi la pili ni Tsh 550,000. Kwa yeyote mwenye kuhitaji fursa hii akachukue fomu Shirika la Elimu Tanzania, application form ni Tsh 20,000 na deadline ni tarehe 30 Septemba 2014″.
TPDC inapenda kuwaeleza Watanzania kuwa habari hizo si za kweli na kwamba TPDC haijafanya makubaliano yoyote na Shirika la Elimu kuhusu suala hilo. TPDC inawaasa Watanzania kuchukua tahadhari ya matangazo ya aina hiyo na inapotokea, tafadhali wasiliana nasi kwa namba za simu zilizooneshwa hapo nchini.
IMETOLEWA NA
KITENGO CHA MAWASILIANO,
SHIRIKA LA MAENDELEO YA PETROLI TANZANIA
                  BWMPensions Towers, TowerA,
                    Junctionof Azikiwe /JamhuriStreets
                  P. O. Box2774,
                  Tel: +255 22 2200103/4
           Dar-es-Salaam, Tanzania

No comments: