Thursday, September 18, 2014

TAMASHA LA KWANZA LA MAGARI LA AUTO MOBILE CLINIC.

Kampuni ya Jast Tanzania Limited kwa kushirikiana na Jossekazi Auto Garage and General supplier wameandaa tamasha la kwanza la Magari la aina yake, linalojulikana kwa jina la Automobile Clinic, ambalo lin
atarajiwa kufanyika kwa siku mbili mfululizo katika viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam.


      Tamasha hilo limelenga katika kutoa huduma ya kitaalamu ya kiufundi kwa wenye magari (Checkup and Fix) kutoka kwa mafundi stadi ambao wamebobea katika fani ya ufundi wa makenika katika aina tofauti tofauti za magari. 



      Akizungumza na vyombo vya habari, kwenye ukumbi wa habari Maelezo, Joseph Mgaya mmiliki wa Jossekazi Auto garage amesema tamasha hili lina lengo kuwakutanisha mafundi stadi na wenye magari, kwa gharama nafuu sana ya shillingi elfu ishirini tu. 


       Mgaya alisema huduma hizo ambazo zilipaswa kugharimu kiasi kikubwa sana cha pesa kwa wenye magari, kitatolewa kwa bei nafuu ili kwa makusudi tu ya kukutanisha mafundi hao na wenye magari,.


       Alisema pamoja na Wateja kutengenezewa Air condition na kujaziwa gesi, kufanyiwa Electronical scan diagnosis, Kuchekiwa Matairi, kuchekiwa Battery, na kupata ushauri wa kiufundi kuhusu gari zao, pia tamasha hilo litakuwa ni sehemu ya kukutanisha watu na kupata burudani.  


       Mgaya alisema, Mafundi wapatao 50 waliobobea katika fani ya ufundi magari, wamepatikana baada ya kufanyiwa usaili wa kina na kupitia mchujo na semina elekezi ili kuweza kuhudumia magari yanayokadiriwa kufika zaidi ya 6000 kwa siku hizo mbili.


      Pamoja na hayo, Mgaya alisema “ Tumeandaa warsha maalum kwa kina dada, tunatambua kuwa asilimia kubwa ya waendesha magari barabarani hivi sasa ni kina dada, tunataka waelewe ni nini cha kufanya pindi atakapopatwa na hitilafu kwenye gari mabarabarani. “ 


        Elimu hii ambayo wameiita ‘Auto First Aid’, alisema itasaidia kupunguza uharibifu zaidi kwenye magari yao,  alisema wakati mwingine kwenye deshboord ya gari kuna kuwa na alama za hatari, lakini kwa kuwa gari inatembea wanawake wengi wamekua wakipuuzia alama hizo na matokeo yake wanasababisha hasara kubwa zaidi.


         “Pamoja na kuwafundisha alama za hatari na nini cha kufanya pindi waonapo alama hizo pia Tutawafundisha kubadilisha matairi, na nini chakufanya na kuwa nacho ikitokea gari limewaharibikia njiani. “ alisema Mgaya. 


        Mgaya ambaye amefanikiwa sana katika ufundi wa AC za magari, Ndege, na Meli, aliongeza kuwa fani ya ufundi makenika ni kazi ya kuheshimika kama zilivyo kazi nyingine, na kuongeza kuwa anaiona fursa kubwa kwa vijana wanaomaliza elimu ya juu.


       “Siku hizi magari yote kuanzia Mwaka 2005 kwenda juu yanatumia vifaa maalum vya computer na internet, pamoja na kuwa maelezo yanakuja kwa lugha ya kingereza, ufundi spana wa kurithishwa hivi sasa hauna nafasi,”alisema.


         “Tofauti na zamani ukifeli form 4, unapelekwa kwenye ufundi hali hivi sasa imebadiliilka fani hii inahitaji wasomi na watu wanaoweza kubadilika na kurudi shuleni kila mara, kama computer matoleo ya magari kila mwaka yanakuja na vitu tofauti, hivi sasa break hazina annoying sound, break zikiisha utaona kwenye dashboard, kutengeneza lazima useme user manual ya kingereza na u download soft ware kwenye internet,” alisema Mgaya na kusistiza vijana waingie kwenye fani hii.  


          Aidha Mkurugenzi wa Jast Tanzania Limited, Jahu Mohammed Kessy, Mratibu wa Tamasha hilo walisema kuwa, Automobile Clinic litakuwa zaidi ya Tamasha. 


     “Katika kuhakikisha tunautumia muda wa wateja wetu vizuri, wakati gari inafanyiwa ufundi, kutakuwa na huduma nyingine za ziada zitakazo patikana siku hizo mbili, kutakuwa na vinywaji, vyakula kama nyama choma, na michezo ya watoto, kutakuwa na huduma ya kulipia ya kuoshewa magari, kusafishiwa taa, na baadhi ya vifaa kama Fire extinguisher, manukato ya gari, Triangle na kadhalika vitauzwa hapo uwanjani,”  


        Jahu alisema Tiketi zitauza kabla, na kwamba tiketi hizo zitakuwa katika mfano wa sticker ya kubandika kwenye magari, na zitapatikana katika vituo vyote vya kuweka mafuta vya TSN, Supermarket zote za TSN, Kwenye ofisi za Millembe insurance, Bon to shine, BM hair cutting salon, na Mlimani City. 


         “Hakutakuwa na Kiingilio kwa watu, lakini badala yake kwa magari, magari yenye sticker pekee ndiyo yatakayoruhusiwa kuingia na kupata huduma hizo, tunashauri wenye kununua sticker wafike mapema kwani watakao fika kwanza ndio watakao hudumiwa,”


         Jahu alisema katika kurudisha kwa jamamii, mafundi hao hamsini baada ya Tamasha watatembelea kwenye hospitali ya CCBRT kusaidia wakina mama wenye matatizo ya fistula.
Tamasha hilo limedhaminiwa na Milembe insurance, Wambi lube oil distributor, TSN, Binslum tires company Limited, I view, Cocacola, Dreams Limited, Hugo Domingo, Olduvai Bay Wash, 0-60 autogarage, Meku Auto spear part, Dick Sound, Brand Tiger, Clouds FM, Auto Beats, Neh Catering, Pamoja na Lim Painting and decorating.

No comments: