Meneja mkuu wa Tigo Tanzania DIEGO GUTIERREZ akizungumza na wanahabari mapema leo juu ya huduma hiyo |
Kampuni ya mawasiliano ya TIGO Tanzania leo
imetangaza kutoa gawio la kiasi cha shilingi billion 14.25 sawa na dola za
kimarekani 8.7 lililolimbikizwa katika account yake ya fedha ya tigo pesa kwa ajili ya wateja
wake.hii inafanya kampuni hiyo kuwa mtandao wa kwanza wa simu duniani kutoa
gawio la fedha kutokana na huduma ya kutuma na kutoa fedha.
Acount
ya mfuko wa fedha wa tigo pesa TIGO PESA TRUST ACCOUNT ni account ambayo fedha
za tigo pesa zinakusanywa na kuhifadhiwa toka huduma ya tigo pesa ilipoanza
miaka minne iliyopita.Kwa sasa TIGO ipo
tayari kutoa gawio la fedha hizo ambazo zilikuwa zinazaa faida baada ya
kuridhiwa na benk kuu ya Tanzania BOT kwa barua rasmi ya kutokuwa na pingamizi
iliyopokelewa julai mwaka huu.
Akizungumza
na wanahabari leo meneja mkuu wa TIGO Tanzania DIEGO GUTIERREZ amesema kuwa gawio hilo la
faida litawanufaisha wateja wote wa tigo wakiwemo mawakala wakuu mawakala wa
reja reja na mteja mmoja mmoja mtumiaji wa tigo pesa.
Aidha amesema kuwa wastani wa faida ambayo mteja
yeyote ataweza kupata inatofautiana na wastani wa fedha ambayo ataweza kubaki
nayo kwenye account yake ya tigo pesa kwa siku kwa hiyo viwango vinatofautiana
kati ya wakala mkuu,wakala wa rejareja na mteja mmoja mmoja.
Gawio hilo litawanufaisha zaidi ya wateja million
3.5 wa tigo pesa nchini wakiwemo mawakala wakuu,mawakala wa reja reja.
No comments:
Post a Comment