Monday, September 15, 2014

WAFANYAKAZI WA BENKI YA NBC WAJIMWAGIA MAJI BARIDI KUCHANGISHA FEDHA KUPAMBANA NA UGONJWA WA FISTULA.

Kaimu Mhazini Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Ivan Tarimo (kushoto) akimwagiwa maji baridi na mmoja wa mfanyakazi mwenzake katika hafla ya kumwagiana maji baridi iitwayo ‘Ice Bucket Challenge’ yenye makusudi ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake wanaosumbuliwa na ugonjwa wa fistula. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Mussa Jallow (katikati) naye akimwagiwa maji baridi ili kutimiza azma ya benki hiyo katika kutafuta fedha ili kusaidia wanawake wanaosumbuliwa na tatizo la ugonjwa wa fistula nchini.


kaimu ofisa mwendeshaji mkuu wa benki ya nbc, Jamie Loden akijimwagia maji baradi ili kusaidia harakati za benki hiyo kuchangisha fedha katika tukio hilo liitwalo ‘Ice Bucket Challenge’ kusaidia wanawake wanaokabiliwa na ugonjwa wa fistula. Kiasi cha fedha kitakachopatika kitapelekwa katika Hospitali ya CCBRT kwa madhumuni hayo.  
Unaweza kuona kama mzaha Fulani lakini ndivyo ilivyokuwa kwa maofisa hawa wa NBC walipoamua kushiriki tukio la ‘Ice Bucket Challenge’ na kumwagiana maji baridi ili kuchangisha fedha kusaidia wanawake wanaosumbuliwa na ugonjwa wa fistula nchini. 

 Baadhi ya wakazi wa jiji waliojitokeza kushuhudia tukio la Ice Bucket Challenge la benki ya NBC wakiwa hawaamini macho yao wakati wafanyakazi wa benki hiyo walipoamua kujimwagia maji baridi ili kutafuta fedha kusaidia wanawake wanaosumbuliwa na ugonjwa wa fistula.

Mkuu wa Rasilimali Watu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Flora Lupembe (kulia) akimwagiwa maji baridi na Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Rukia Mtingwa katika hafla ya kumwagiana maji baridi iitwayo ‘Ice Bucket Challenge’ yenye makusudi ya kuchangisha fedha kwa ajili kusaidia wanawake wanaosumbuliwa na ugonjwa wa fistula. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.

No comments: