Mtangazaji wa zamani wa Radio Tanzania Dar es salaam(RTD) ambayo sasa ni TBC Taifa, Ben Hamis Kikoromo au maarufu Ben Kiko (pichani) amefariki duania.
Mwandishi huyo mkongwe nchini Ben Kiko amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hosptali ya taifa ya rufaa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Ben Kiko alihamishiwa katika hosptali ya Muhimbili kutokea hosptali ya Jeshi ya Milambo ya mkoani Tabora ambako alilazwa kwa ajili ya matibabu ya figo kwa muda wa wiki mbili.
Atakumbukwa kama mmoja wa watangazaji mahiri ambao walijipatia umaarufu mkubwa ambapo katika enzi za uhai wake alifanya makubwa wakati wa Vita vya Kagera kwa kuleta matukio mbalimbali kutoka uwanja wa vita. Pia aliupaisha sana mkoa wa Tabora alikokuwa akifanyia kazi kwa habari na visa mbalimbali katika kipindi cha RTD cha Majira.
MUNGU ILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA, AMIN
No comments:
Post a Comment