Monday, November 3, 2014

HABARI ILIYOTIKISA JIJI--PAUL MAKONDA AIBUKA ,AJIBU TUHUMA ZA KUDAIWA KUMPIGA JAJI WARIOBA--SOMA HAPA


Na Karoli Vinsent
SIKU moja kupita Baada ya  aliyekuwa  Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba,  Paul Makonda kumrushia Chupa aliyekuwa Mwenyekiti wa tume ya ukusanyaji Maoni ya Katiba  Jaji Joseph Warioba wakati wa mdahalo wa kutoa elimu kuhusu Katiba iliyopendekezwa na bunge Maalum la Katiba
 ,         Mjumbe huyo ameibuka na kusema  taarifa  zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari, kuhisika na vurugu kwenye Kongamano la  kutoa elimu ya katiba inayopendekezwa  zilikuwa na lengo la uchonganishi.
            Na pia , amekanusha kumpiga jaji Warioba, huku akisema waliofanya vurugu hizo jana, katika Ukumbi wa Mikutano wa Blue Peal, ni kundi la watu lisilofahamu demokrasia na lina nia ya kuchafua taswira ya nchi.
         Makonda akizungumza kwa uchungu alisema wakati baadhi ya vijana wakianza kurusha viti alilazimika kumtoa katika ukumbi aliyekuwa mjumbe mwenzake wa bunge hilo, Amon mpanju ambaye ni mlemavu wa macho ili hasizurike na fujo hizo.
              Hayo yamesemwa Makonda leo Jijini   Dar es Salaam wakati wa Mkutano na waaandishi wa Habari , ambapo alisema wakati akimtoa, Mpanju alifuatwa na  Jaji Warioba akiwa na  Prof. Paramagamba Kabudi, kujaribu kutuliza vurugu hizo lakini hawakuweza kufanikiwa.
           Makonda ambaye pia ni Kiongozi wa uhamisishaji kutoka ndani ya chama  cha Mapinduzi CCM alisema Baada ya hali kuwa mbaya ukumbini hapo, Jaji warioba alimtaka kuhakikisha anamfikisha, Mpanju mahali salama huku wakijaribu  kurudisha hali ya usalama ukumbini hapo.
          Aliongeza kuwa, wakiwa wanaondoka kupitia nyuma ya jukwaa alifuatwa naaliyekuwa mtangazaji wa radio ya Clauds Fm ambaye sasa ni  mwandishi wa Shirika la Utangazaji la Uingereza, Anord  Kayanda, akiwa amejeruhiwa kichwani akimtaka kumsaidia.
     Makonda alisema, ghafra kundi la watu lilimvamia na kuanza kumshambulia hali iliyomfanya kuwaita walinzi kumwondoa jaji Warioba pamoja na Mapanju.
         “Nilisika sauti za watu wakisema tumpige Makonda, huyu ndiye aliyeandika katiba yenyewe, hivyo nilimsihi Mzee Warioba akimbie” alisisitiza Makonda.
           Kutokana na kundi hilo kuzidi kumshambulia, Makonda alisema aliamua kukimbia hadi vyombo vya usalama vilivyofika kutoa msaada.
           Alisisitiza kuwa , yeye alifika kwenye mkutano huo kama mwananchi wa kawaida kusikiliza kile kilichokuwa kikijadiliwaa.
      Akizungumzia tuhuma za kuongoza vijana waliokuwa wamebeba mabango kwenye mdahalo huo, alisema hakuwa akiwasiliana na mtu yeyote akiwa ndani ya mdahalo huo.
Alisema kama angekuwa anawaongoza vijana hao, asingeweza kupigwa hivyo shutuma hizo hazina ukweli wowote.
Katika kongamano hilo lililoandaliwa na taasisi ya Mwalimu Nyerere, 
         polisi walilazimika kuingila kati kumnusuru Jaji Warioba na kulivunja kutokana na kuchafuka kwa hali ya usalama.


    Kwa upande wake Msomi na mchambuzi wa Masuala ya Kisiasa kutoka chuo Kikuu cha Dodoma Seiph Yahaya alisema Makonda hana cha kujitetea kwa watanzania kwa kitendo chake hakikubaliki na mtu yeyote na akakitaka chama cha Mapinduzi CCM kimvua uongozi Makonda kwa kitendo cha utovu wa nizamu aliyofanya kwani chama cha mapinduzi kinasifika barani afrika kuwa na viongozi wenye tija huku ikizingatia chama hicho kimsaidia nchi nyingi

No comments: