Ikiwa ni siku kadhaa baada ya rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania dk JAKAYA KIKWETE kuzungumza na taifa kuhusu sakata la
uchotwaji wa fedha za account ya TEGETA ESCROW.Nao umoja wa katiba ya wananchi
UKAWA wameibuka na kumvaa rais kwa kile walichokiita ni hotuba ya
kulifedhehesha taifa kwani imeonyesha wazi kuwatetea wahusika wakuu wa sakata
hilo.
Wakizungumza na wanahabari muda huu jijini Dare s salaam
mwenyekiti mwenza wa umoja huo ambaye ni mwenyekiti wa CUF profesa IBRAHIM
LIPUMBA amesema kuwa hotuba ya rais kikwete ni hotuba mbovu na imelenga wazi
wazi kuuficha ukweli wa sakata hilo kwa kuwatetea wahusika hao huku akisema
umoja wao hautachoka kulipigania swala hilo hadi mwisho.
Profesa lipumba anasema kuwa ni jambo la ajabu kuona
kuwa rais anashindwa kuwachukulia hatua kali wahusika kama mmiliki wa PAP
singasinga HARBINDER SINGH pamoja na james rugemarila ambao kwenye kamati na
report zote wanatajwa kuwa wao ndio waliohusika katika mchakato huo wa
uchakataji wa pesa hizo
Profesa LIPUMBA akizungumza na wanahabari |
“hivi huyu singasinga ana nini,amempa nini rais,yani
ameiweka serikali mkonono au mfukoni,maana rais hataki hata kumgusa,ni jambo la
kustajaabisha sana kuona rais anawanyamazia wawekezaji wezi kama huyu ambao
wanawaibia watanzania mchana kweupe”alihoji lipumba
Aidha amesema kuwa ni lazima rais ajue kuwa kazi yake
sasa ni kutekeleza maamuzi ya bunge ambayo yalipitishwa na wabunge wote kwa
umoja wao na waziri mkuu akiwemo na sio kuanza kufanya uchunguzi upya kwani
uchunguzi ulishafanyika kinachotakiwa sasa ni utekelezaji tu.
UKAWA wamesema kuwa pamoja na hotuba aliyoitoa rais
pamoja na kuwawajibisha watu kadhaa bado haitoshi kwani bado kuna watu wengi
ambao wamehusika na sakata hilo na liko wazi hivyo wafikishwe mahakamani mara
moja kwa ubadhilifu wa mali ya umma.
“Tunataka yafuatayo yafanyike, kwanza kikao kijacho
cha bunge kiwawajibishe serikali kwa kushindwa kutekeleza maazimio yao.ukawa
tutaendelea kuwaelimisha wananchi kuhusu sakata hilo,hatua za kisheria
zichukuliwe kwa wote waliohusika,pia sheria ya maadili itungwe upya iweke wazi
mali za viongozi wetu wa umma”ameongeza lipumba.
Katika hatua nyingine UKAWA wametangaza kuitisha
maadamano na mikutano nchi nzima kama serikali itaendelea kuwatetea wezi wa
fedha hizo za watanzania,kulenga kufikisha ujumbe kwa wananchi kuhusu ukweli wa
sakata hilo na hatua ambazo zinachukuliwa na serikali kwa sasa
No comments:
Post a Comment