Wednesday, December 31, 2014

JESHI LA POLISI LIMEJIPANGA KIKAMILIFU KUHUSU MKESHA WA MWAKA MPYA WA 2015

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limepanga mikakati madhubuti ya kuhakikisha kwamba mkesha kuelekea Mwaka Mpya 2015 unakuwa salama, sherehe za mwaka mpya, kuandamana, baadhi ya watu wachache hasa vijana hupenda kuchoma matairi barabarani, kulipua fataki na vurugu za kila aina kwa lengo la kuonyesha furaha yao ya kuingia mwaka 2015.

Hali kama hiyo haitavumiliwa na Jeshi la Polisi kwa sababu badala ya sherehe hugeuka vitisho, vurugu, na kisha kuwatia hofu wananchi wasiokuwa na hatia. Katika harakati hizo Jeshi limeweka mpango kazi utakaowashirikisha askari wa vikosi vyote pamoja na wadau mbalimbali watakaojihusisha na ulinzi siku hiyo. Watakaojihusisha na ulinzi ni pamoja na kikosi cha Zimamoto, kampuni binafsi za Ulinzi, na katika Jeshi la Polisi kutakuwa na kikosi cha FFU na kikosi cha Mbwa na Farasi.




Kampuni binafsi za Ulinzi zitashiriki kikamilifu katika ulinzi huo ambapo watafanya doria za miguu kwa pamoja, doria za magari, pamoja na askari wa pikipiki. Baadhi ya watu hupenda kusherehekea mwaka mpya katika nyumba za ibada ambapo Jeshi la Polisi litatoa ulinzi. Kutakuwa na ulinzi katika fukwe za bahari pamoja na sehemu zote ambazo zinzkuwa na mikusanyiko ya watu wengi kama vile katika Hotel kubwa kubwa na sehemu za wazi. Uwanja wa Taifa utalindwa kutokana na mikusanyiko mkubwa wa watu utakaokuwepo siku ya mkesha pamoja na viwanja vingine vyote vyenye mikusanyiko mingine kama hiyo.


Magari ya Zimamoto yatafanya doria yakisindikizwa na Jeshi la Polisi ili kuhakikisha kwamba yeyote atakayejaribu kuchoma moto matairi au gari atakamatwa na moto unazimwa.

Kutakuwa na ulinzi wa kutosha ufukweni mwa bahari ambapo Boti za Polisi zitafanya doria ili kuwabaini wahalifu wa aina yoyote kutoka Baharini au nje watakaojaribu kuingia na kufanya uhalifu jijini.


Helkopta ya Polisi itaanza doria kuanzia saa kumi na mbili jioni ili kukagua maandalizi yoyote ya uchomaji moto au uhalifu mwingine wa aina yoyote. Wananchi wanashauriwa kuwa makini na familia zao na hasa watoto wadogo wasiruhusiwe kuingia barabarani wakati wa sherehe hizi kwani ni hatari kwa maisha yao.


Madereva wajiepushe na ulevi ambao wanaweza kusababisha ajali zisizo za lazima pindi wanapoendesha vyombo vya moto katika kipindi hicho. Maafisa, Wakaguzi na Askari watakuwa “standby” kwa shughuli za ziada. Aidha, kutakuwa na mwonekano wa askari wengi wa kila aina kabla na wakati wa sherehe hizo ili kuhakikisha kwamba kuna amani na utulivu wakati wote wa kuingia mwaka 2015.

Wananchi wanaaswa kujihadhari na kufanya vitendo visivyo vya kawaida kama vile kufyatua risasi za moto, kuendesha magari kwa mwendo kasi sana, kupiga honi hovyo, au magari kuwa na milio ya kutisha yenye kero na badala yake wafuate taratibu pamoja na kutii sheria bila shuruti.


Kinyume cha maagazo tajwa hapo, mtu yeyote atakayekaidi na kufanya makosa ya jinai atachukuliwa hatua za haraka na hatimaye kufikishwa katika vyombo vya sheria kwa mashtaka dhidi yake.


Ni muhimu pia wadau mbalimbali pamoja na wananchi kwa jumla kutoa taarifa wakati ambapo kuna ishara ya uvunjifu wa amani au wakiwaona watu wanaowatilia mashaka watoe taarifa kwa namba zifuatazo:


1. ZCO - Constantine Masawe – SACP:   0713-510 856 / 0658-111 100

2. RPC ILALA – Mary Nzuki – SACP:     0715-009 980 / 0754-339 558

3. RPC TEMEKE – Kihenya Kihenya – SACP: 0715-009 979 / 0754-397 454

4. RPC K’NDON– Camillius Wambura – ACP:  0715-009 976 / 0684-111 111


S. H. KOVA,

KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM,

DAR ES SALAAM.


JEHI LAPOLISI LIMEJIPANGA KIKAMI

LIFU KUHUSU MKESHA WA MWAKA MPYA WA 2015

No comments: