Baadhi ya wanafunzi waliojitokeza katika maadhimisho hayo leo jijini Dar es salaam |
Kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC kwa
kushirikiana na wadau wengine wa haki za binadamu leo wameadhimisha miaka 66
tangu kuanzishwa kwa tamko la haki za binadamu la ulimwengu ambalo
lilitoka tarehe 10,mwezi wa 12 mwaka 1948,tamko ambalo ndio hasa chimbuko la
misingi ya haki za binadamu kote duniani.
Tamko hilo ambalo linaainisha haki za
kiuchumi,utamaduni,kiraia n kijamii lilifwatiwa na mikataba miwili ambayo ni
mkataba wa kimataifa wa haki za kiraia,pamoja na mkataba wa kimataifa wa haki
za kiuchumi,kijamii,na utamaduni 1966.
Akizungumza katika maadhimishohayo ambayo awali
yalitanguliwa na maandamano ya wadau wa haki za binadamu kaimu mkurugenzi wa
LHRC Ezekieli Masanja amesema kuwa ipo haja ya serikali kuanza kuweka masimo ya
haki za binadamu katika mitaala ya shule za msingi ili kuanza kuwajengea
wanafunzi uelewa mapema wa haki za binadamu na jinsi ya kuzilinda,ikiwa ni
pamoja na kukuza uelewa wa vijana wa shule juu ya haki za binadamu.
Kwaya mbalimbali zikitoa burudani |
Amesema kuwa pamoja na mambo yote kufanyika lakini bado kna haja kubwa ya kuanza kujenge uelewa
wa vijanawadogo juu ya haki za binadamu wakiwa shuleni.
Aidha LHRC wametoa tathimini yao ya haki za binadamu kwa
Tanzania ambpo bado inaonyesha zipo changamoto kubwa za ulindaji wa haki hizo
mfano maeneo kama kiwango cha elimu bado kipo chini kwa watanzania,migogoro
hasa ya ardhi bado imeendelea kuwa tatizo kwa watanzania,pamoja na ajali za
barabarani na mauaji mbalmbali yameendlea kuwa changamoto kubwa kwa watanzania.
kaimu mkurugenzi wa LHRC Ezekieli Masanja |
Burudani |
No comments:
Post a Comment