Tuesday, December 30, 2014

SIRI YA PHIRI KUTIMULIWA SIMBA SC HII HAPA.SOMA

Wachezaji wa Simba raia wa Kiganda ndio wamemponza kocha Mzambia
Patrick Phiri kufungashiwa virago ndani ya klabu hiyo ya Msimbazi huku Mserbia Goran
Kopunovic akitarajiwa kutua rasmi kesho Jumatano.


Habari za uhakika kutoka Simba zinasema kuwa uongozi wa klabu hiyo chini ya
mwenyekiti wake Evans Aveva uliketi juzi usiku majira ya saa mbili na kikao kumalizika
saa saba usiku kwa maazimio ya kumfukuza Phiri na jana jioni alikabidhiwa rasmi barua
yake ya kuachishwa kazi na nafasi yake kuchukuliwa na Serbia, Goran Kopunovic.



Chanzo hicho kinasema kuwa matokeo mabovu dhidi ya Kagera ndio yamemponza Phiri
kutimuliwa hasa baada ya kukaidi agizo la viongozi la kumtaka kocha huyo asiwapange
wachezaji wote waganda.


"Kocha aliambiwa panga wachezaji alioenda nao Zanzibar na kufanya nao mazoezi kuanzia
siku ya kwanza, akambiwa hata 'sub' (mabadiliko) wasiwepo lakini yeye alipomuona Okwi
akaanza kushangilia mechi ya Kagera kapanga wachezaji aliotaka yeye matokeo yake timu
ikafungwa.


Wachezaji waganda waliomponza Phiri ni Joseph Owino, Emmanuel Okwi, Dan
Sserunkuma, Juuko Murshid na Simon Sserunkuma.


Akizungumzia suala hilo Phiri alisema "Nipo tayari kupokea lawama zozote nilishasema
toka mwanzo, wao wameamua hivyo mimi sina jinsi ingwa mpaka muda huu (saa saba
mchana jana) Aveva (Mwenyekiti wa Simba) hajaniambia chochote.


"Ila najua kila kinachoendelea, najua wameshatoa uamuzi ya kunifukuza nasubiri Aveva
aniambie rasmi, najua walikuwa na kikao, kuna mtu mmoja alinipigia na kunieleza kila kitu
kilichokuwa kinaendelea kwenye kikao chao na uamuzi waliyochukua, nipo tayari nasubiri
tu uongozi uniambie rasmi." alisema na kudai kuwa iwapo uongozi hautampa barua ya
kuvunja mkataba wake ataendelea na mazoezi leo kwenye uwanja wa TCC na mchana
ataelekea Zanzibar kwa ajili ya michuano ya Kombe la Mapinduzi.


Hata hivyo mmoja wa viongozi wa Simba alisisitiza tayari wameshaafikia kuvunja mkataba
na Phiri na kumlipa mshahara wake wa miezi miwili kama fidia ambayo ni dola 10,000.
Phiri amekuwa akilipwa dola 5,000 kwa mwezi.


Kiongozi huyo pia alidai kuwa timu hiyo itaenda Zanzibar ikiwa chini ya kocha msaidizi
Selemani Matola. 


Katika hatua nyingine ya mastaa watatu wa klabu hiyo wametimua nchini Uganda kutaka
fedha zao na si mali kauli.
Habari za kuaminika kutoka ndani ya klabu hiyo
ya Msimbazi zinasema kuwa Waganda
hao wamekwea pipa jana asubuhi wakishinikiza uongozi wa Simba uwape fedha zao.


"Owino ana mgogoro na viongozi kwa vile aligoma kusaini mkataba akishinikiza
arekebishiwe maslahi yake uongozi haukufanya hivyo Owino akagoma kusaini, viongozi
ndio wamemuwekea bifu hawataki apangwe kwenye mechi,

"Juuko Murshid na Simon Sserunkuma wao wanadai fedha zao za usajili na mpaka sasa
uongozi unawazungusha.


Blog ya Jamii iliwatafuta viongozi wa Simba kwa nyakati tofauti akiwemo mwenyekiti wa
kamati ya usajili Zakaria Hans Pope lakini simu yake ilikuwa ikiita kwa muda mrefu bila
kupokelewa hali kadhalika kwa Mwenyekiti wa klabu hiyo Evans Aveva na katibu mkuu
Steven Ally.

No comments: