Saturday, December 27, 2014

TANDALE SACCOS WAFANYA MKUTANO WAO MKUU WA MWAKA

Maelfu ya wanachama wa TANDALE SACCOS waliojitokeza katika mkutano wake mkuu uliofanyika leo jijini Dar es salaam 
Chama cha akiba na mikopo SACCOS kilichopo Dar es salaam kinachokwenda kwa jina la TANDALE SACCOS leo kimefanya mkutano wake mkuu wa mwaka ambao mkutano huo umefanyika katika hoteli ya lunch time magomeni jijini Dar es salaam mkutano ambao pia umetumika kuchagua viongozi wapya wa chama hicho ambacho kinatajwa kama SACCOS bora ndani ya jiji la Dar es salaam

Katibu wa bodi ya SACCOS ya TANDALE SACCOS Bi ZENA KAITILA akizungumza na wanahabari wakati wa mkutano wa mwaka wa chama hicho ambapo amesema kuwa chama hicho sasa kimetimiza zaidi ya wanachama hai elfu tisa,,ambapo ni idadi kubwa sana kulinganisha na baadhi ya SACCOS nyingine jijini dae es salaam.

Bi ZENA amesema kuwa hadi sasa wana mtaji wa zaidi ya bilioni moja na wanachama wake kwa sasa wana uwezo wa kukopa hadi milioni hamsini kwa mara moja kutokana mapato yao kuwa mazuri.

Amesema pamoja na mafanikio hayo bado changamoto hazikosekani ambapo amesema kuwa moja ya changamoto hizo ni pamoja na kuwa na wanachama ambao wamekuwa sio wanachama hai ambao wamekuwa wakishindwa kuchukua mkopo  na kurudisha kwa wakati jambo ambalo limekuwa ni chanagamito kubwa kwa chama chao

Hadi mtandao huu unaondoka katika eneo la tukio chama hicho kilikuwa katika uchaguzi wa viongozi wao wapya na hapa ni viongozi mbali mbali wa chama hicho wakipongezana baada ya kuchaguliwa kukiongoza chama hicho


No comments: