Pichani ni Meneja Mradi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) Mhandisi Kapuulya Angetile Musomba akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar Es Salaam Picha na Seleiman Magari |
NA KAROLI VINSENT
SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeweka wazi gharama za Mradi wa ujenzi wa Bomba la Gesi asilia kutoka Mkoani Mtwala,songosongo-Lindi na Pwani hadi Dar ES Salaam,ambapo wamesema mradii huo unatarajia kugharimu pesa za kimarekani Dola Bilioni 1.2 sawa na fedha za kitanzania zaidi ya Trilioni 1.2.
Kuibuka huku kwa (TPDC)kumekuja siku chache kupita baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe, wakati alipokuwa akichangia Bungeni Dodoma aliitupia Lawama Shirika hilo kwa Madai limefanya usiri wa Mkataba wa ke wa Gesi na kupelekea kuwepo na ufisadi wa zaidi ya pesa za kitanzania Trilioni 1.
Akiweka bayana Gharama hizo za mradi leo jijini Dar es Salaam Wakati wa Mkutano na Waandishi wa habari, Meneja Mradi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) Mhandisi Kapuulya Angetile Musomba amesema garama za mradi wa bomba hilo ni Dola Bilioni 1.2 ambazo ni sawa na pesa za kitanzania zaidi ya Trilioni 1.2.
Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Meneja wa Mradi wa TPDC Mhandisi Musomba |
Kati ya pesa hizo Benki ya Exim ya China imechangia Asilimi 95 na serikali ya Tanzania alimia 5.
Mhandisi Musomba aliongeza kuwa Kiasi hicho cha Fedha kinatumika kugharamia maeneo mbalimbali ikiwemo-
Mtambo wa kusafisha gesi asilia ya songo Songo inayogaramia Dola za kimarekani 151,735000,na mtambo wa kusafisha gesi asilia wa Mnazi bay pia unagarimu Dola za Kimarekani 197,877,000.
Aidha,Mhandisi Musomba alisema mradi huo umefikia asilimia 94 katika kukamilika kwake na mradi wenyewe unatarajia kukamilika kwake Mwezi wa sita mwaka huu.
Mradi huo wa Gesi ukikamilika kwake utasaidia kuwaletea faida kubwa wananchi ikiwemo katika kupata umeme wa uhakika ,kupanua viwanda,utunzi wa mazingira,upatikanaji wa Ajira,maji safi pamoja na matumizi ya gesi ambapo Bomba hilo la Gesi litapitia.
No comments:
Post a Comment