Saturday, January 24, 2015

MPYAAA---YAMETIMIAA MUHONGO AJIUZULU RASMI



HABARI zilizotufikia  mda huu zinasema Hatimaye  Waziri wa Nisharti na Madini Profesa Sospeter Muhongo  amejiuzulu katika nafasi aliyokuwa nao .
         Kwa mujibu wa Mwandishi wa Mtandao huu KAROLI VINSENT aliyekuwepo  Makao Makuu ya Wizaya ya Nishati na Madini iliyoko posta jijini Dar es Salaam ambapo ndio kuna mkutano na waandishi wa Habari uliohitishwa mahususi kuzungumzia Hatima yake. 

Anasema Profesa Huyo msomi wa masuala ya Miamba nchini Ameamua Kuachia ngazi nafasi yake akidai anawaachia wengine kwenye Nafasi hiyo kutokana  na watu waameacha kuzungumzia masuala ya maendeleo wanazungumzia mambo ya Escrow huku yeye hahusiki.
  
  Profesa muhongo aliongeza kuwa  hata mkataba wa Escrow ambao ndio umeleta yote hayo anasema yeye hakuwepo wakati mkataba huo unasahiniwa.
    
  “Mimi nashangaa leo watu kila kona naona mimi ni mwizi, yaani kama mimi ndio nimechukua mabilioni ya escrow wakati ukweli hupo wazi wakati wizara ya nisharti inaingia mwenye mkataba huo mimi sikuwepo kwenye nafasi ya uwaziri,lakini leo watu bado wananiona mimi ni mwizi”
   
    “Acha niaachia ngazi nafasi hii ya uwaziri kwani imekuwa ni shida sana, mimi ni  mtu msomi nimepata tuzo sehemu mbalimbali duniani nasifika kwa kutoa ushahuri wenye tija,lakini leo naonekana mwizi,wakati kiihistoria yangu mimi ni mtu msafi sina doa na wala sijawai hata kumwibia mtu,lakini watu wananiona mimi mwizi”alisema Profesa Muhongo.
    
 Aidha,Profesa Muhongo alisema kabla hajafikia hatua ya kutangaza kujiuzulu aliwasiliana  na Rais Jakaya Kikwete alimuleze hatua nayotaka kuchukua ya kujiuzulu na Rais akakubali kujiuzulu kwake.
      
  Vilevile Profesa Muhongo aliendelea kukanusha kile kilichotajwa na Ripoti ya PAC iliyomtuhumu kwamba yeye alikuwa Dalali kati ya anayejiita na kuitwa mmiliki wa IPTL ambayo sasa ni PAP Bwana Seith na Mkurugenzi wa VIP Engineering Bwana James Rugimalira na kusema
Kamati hiyo imemuonea.
        
Kujiuzulu huku kwa Profesa Muhongo kunatokana na mashinikizo mbalimbali kutoka ndani ya nchi hususani Bunge pamoja na nchi wahisani ambao waligoma kutoa fedha za Bajeti wakitaka wakiohusika na ufisadi wa Bilioni 320 kwenye Akaunti ya Tegeta escrow iliyokuwa benki kuu BOT wachukuliwe hatua.

ENDELEA KUFUATILIA MTANDAO HUU ULIoSHEHUENI WAANDISHI WALIOBOBEA KATIKA MASUALA YA HABARI UTAPA TAARIFA KAMILI

No comments: