Taasisi ya kimataifa ya uhudumiaji wa bidhaa na uchukuzi
wa bidhaa CILT yani THE CHARTERD INSTITUTE OF LOGISTIC AND TRANSPORT Tawi la Tanzania
imeandaa mkutano mkubwa nchini ambao utafanyika katika mkoa wa arusha tarehe 3
na 4 mwezi wa tatu mkutano wenye lengo la kuwakutanisha wadau mbalimbali wa
maswala ya usafirishaji na uchukuzi kujadili changamoto mbalimbli katika secta
hiyo.
Mwenyekiti wa CILT nchini Tanzania GEORGE MAKUKE akizungumza kuhusu mkutano huo na taasisi hiyo inavyofanya kazi. |
Mkutano huo ambao utafanyika katika hoteli ya mount meru
jijini arusha una mipango pia ya kuwakutanisha wanataaluma wa maswala ya
uchukuzi na usafirishaji wa bidhaa ili kubadilishana uzoefu katika taluma hiyo.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kupata chai yenye
lengo la kuchangisha fedha ambazo zitasaidia katika kuendesha mutano huo
aliyekuwa waziri wa uchukuzi ambaye sasa ni waziri wa ushirikian wa Africa mashariki
MH HARSON MWAKYEMBE amesema kuwa Tanzania kupata nafasi ya kuwa mwenyeji wa
mkutano mkubwa kama huu ni fursa ya kipekee ambayo nchi inatakiwa kujivunia na
kuitumia kujitangaza kimataifa.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo ndugu ZAKARIA HANSPOP akizngumza. |
Amesema kuwa mkutano huo utawasaidia hasa vijana
ambao wanasoma maswala haya kukutana na wazoefu katika fani hiyo na
kubadilishana uzoefu jambo ambalo litawajengea uzoefu katika kazi zao pindi
watakapoingia katika fani.
Aidha mwenyekiti wa CILT nchini Tanzania GEORGE
MAKUKE anesema kuwa kwa sasa katika secta ya usafirishaj wa bidha nchini
kumekuwa na watu ambao amewaita makanjanja ambao wamekuwa hawana weledi katika
kazi na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi jambo ambalo amesema kuwa
linafaa kupigwa vita mara moja.
Katika hatua nyingine
mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo ndugu ZAKARIA HANSPOP akizngumza
katika hafla hiyo amewataka watanzania hususani wadau wa secta hiyo kujitoa
katika kuufadhili mkutano huo kwani una manufaa makubwa katika ukuaji wa secta
ya usafirishaji na uchukuzi nchini Tanzania
Picha tatu za juu zikionyesha washiriki mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo |
No comments:
Post a Comment