Thursday, February 26, 2015

breaking newzz--MSANII CHID BENZ ATUPWA JELA MIAKA MIWILI KOSA LA MADAWA YA KULEVYA

Breaking News:Chidi Benzi atupwa jela Miaka miwili kwa makosa ya kukutwa na Dawa za kulevya aina ya Heroin wakati alipokuwa akienda kufanya tamasha la muziki Oktoba 24 Mwaka jana.





Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Rashidi Abdallah Makwaro Maarufu kama (Chid Benzi) amehukumiwa kifungo cha miaka mwili jela au kulika faini ya shingili laki tisa bada ya kupatikana na hatia ya makosa matatu ikiwemo kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroin yenye thamani ya sh. 38,638, bangi ya sh. 1,720 na vifaa ya kuvutia dawa hizo kijiko na kigae.


Hukumu huyo imetolewa katika mahakama ya hakimu mkazi kisitu na  hakimu mkazi mkuu, Warialwande Lema aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo iliyoanza kusikilizwa Oktoba 18 mwaka jana na msaani huyo Chidi Benzi kukiri makosa yote matatu baada ya kukamatwa na dawa hizo za kulevya oktoba 24, mwaka jana  katika uwanja wa ndege wa julius nyerere akielekea mkoani mwanza kufanya tamasha la muziki wake.


  Chid Benzi-Mwanamuziki Tanzania wakati akipelekwa kizimbani
Awali akisoma mashtaka kabla ya kesi hiyo kusikilizwa wakili wa serikali inspekta Jackson Chidunda,alidai kuwa oktoba 24, mwaka jana katika uwanja wa ndege wa julius nyerere, mshtakiwa alikutwa dawa za kulevya aina ya Heroin isivyo halali zenye uzito wa  gramu 0.85. Katika shitaka la pili, ilidaiwa kuwa siku na eneo la tukio la kwanza, mshtakiwa alikutwa na gramu 1.72 za bangi isivyo halali.


Msanii Chid benzi mwenye umri wa miaka (29 ni moja kati ya wanamuziki wa HipHop wanaofanya vyema katika tasnia hiyo hapa Tanzania ambapo apandapo jukwaani huishiwi hamu ya kumtizama na kupenda anavyofanya kazi zake za kimziki huku akiwa mwenye majina lukuki kama King kong na mengine mengi.

UPDATE---HABARI AMBAZO ZINAUFIKIA MTANDAO HUU ZINADAI KUWA TAYARI MSANII CHID BENZ AMEFANIKIWA KULIPA FAIN YA SHILINGI LAKI TISA NA AMEACHIWA HURU KUENDELEA NA SHUGHULI ZAKE

No comments: