Thursday, February 26, 2015

MASWALI 10 ALIYOYAJIBU JOHN MNYIKA KUTOKA KWA WAPIGA KURA WAKE,TIZAMA HAPA




1. Mengi Athman (30), Machinga; mkazi wa Mburahati.
Ulituahidi kuondoa kero ya machinga kabla ya kupata kura yangu, leo hii tunaishi kama popo mitaani umefanya jitihada gani mpaka sasa?
Jibu: Nimetekeleza ahadi hii kwa namna mbalimbali mwaka 2011, 2012, 2013 na 2014. Nimefanya mkutano wa kikazi na Machinga na kupokea kero zilizopewa  kipaumbele.
2. Omary Sebea (33), Fundi Seremala; mkazi wa Kimara King’ong’o
Miaka mitano imekwisha na kilio kikubwa cha maji bado hakijamalizika, ninanunua ndoo Sh500, kwa nini nikupe kura yangu 2015? Kwanini eneo la King’ong’o maji hayapatikani wakati kuanzia Kimara mpaka Msikitini na Matosa yanapatikana?
Jibu: Miaka mitano haijaisha na tayari kuna maeneo ambayo hakuna kilio cha maji. Nashukuru Omary Sebea ametambua kwamba maji yanafika Kimara mpaka Msikitini na Matosa. Juu ya eneo la King’ong’o na eneo lingine ambalo hajalitaja la Michungwani maji hayafiki na nilifuatilia Dawasa na Dawasco toka mwaka 2010 na 2011 na nikaelezwa kwamba kwa mwinuko uliopo hayawezi kufika kwa urahisi kutokana na mlima. Sikuridhika na majibu hayo hivyo nitaendelea kuisimamia Serikali.
3. Hamad Hussein (27), Dereva Bajaji; Mkazi wa Makoka
Kabla ya kutoa kura yangu, uliahidi kujenga Barabara ya Makoka lakini kwa nini mpaka leo bado haijajengwa?  Tunateseka na hakuna dalili zozote za ujenzi.
Jibu: Nilitekeleza wajibu huo kwa upande wa barabara ya Makoka. Kipande kingine kidogo cha Makoka kitanufaika na ujenzi kwa kiwango cha lami kwa barabara kutoka External kupitia Makoka mpaka Kilungule hadi Kimara ambayo itajengwa kupitia wakala wa Barabara Nchini (Tanroads).
4. Haika Elias (31), Mama Lishe Ubungo.
Mnyika ulituahidi kupata eneo la kudumu kwa ajili ya kufanyia biashara zetu hapa Ubungo, lakini kwa nini tumekuwa tukifukuzwa kama wakimbizi.
Jibu: Kwa upande wa Machinga wa Ubungo Mataa sehemu yao nilipendekeza watengewe eneo kwenye kiwanja ambacho zamani kilikuwa kinamilikiwa na Simu 2000. Hatimaye eneo hilo limejengwa kituo kipya cha mabasi Sinza ambapo kumetengwa pia eneo la wafanyabiashara ndogo ndogo. Hata hivyo, kuna udhaifu katika ugawaji wa maeneo kwa Machinga. Meya wa Kinondoni ameahidi kwamba Manispaa italipatia ufumbuzi.
6. Godfrey Kazi (30) Bodaboda; Shekilango.
Siasa imetuathiri tusiokuwa na hatia, Mnyika kwa nini umeshindwa kutusaidia Bodaboda tufanye biashara kwa uhuru.Kuna dhambi gani kuingia na kutoka katikati ya mji(Posta)?
Jibu: Sheria inayohusika ambayo ni The Surface and Marine Transport Regulatory Authority Act; sheria namba 9 ya mwaka 2001. Haikatazi pikipiki/bodaboda au bajaj kuingia katika maeneo ya katikati ya jiji. . Kama kuna bodaboda bado zinakamatwa kwa sababu hiyo katika maeneo hayo kwa agizo la mkuu wa mkoa naomba nijulishwe nichukue hatua za ziada. Kwa upande wa katikati ya Jiji maeneo ya Kariokoo na Posta nilijibiwa kwamba yapo upande wa Jimbo la Ilala hivyo maamuzi yake yanategemea pia Halmashauri ya Jiji na Manispaa ya Ilala.
7. Nuhu Masanja (45), Msukuma mkokoteni Ubungo
Kwa nini umeshindwa kutekeleza ahadi yako ya kuleta maji Ubungo Kitintale, kwa nini usihukumiwe kwa ahadi hiyo?
Jibu: Suala la maji nitaendelea kulipa kipaumbele kuwa ni kero kuu ya wananchi siyo wa Kitintale tu bali kitaifa hivyo nakusudia kupeleka hoja nyingine bungeni juu ya ufisadi na udhaifu katika miradi ya maji nchini.
8. Kulwa Chindiye(30), Dereva Teksi;
Kabla ya kuingia madarakani ulituahidi kuunda vikundi vya ujasiriamali ili utupatie mikopo, tuliunda vikundi lakini kwa nini mpaka leo hatujapata?
Jibu: Ahadi hii nimeitekeleza kwa njia na viwango mbalimbali. Orodha ya vikundi vilivyopata mikopo inapatikana katika ofisi ya mbunge Ubungo. Baada ya kulipigania hilo nashukuru kwa mara ya kwanza kwenye historia ya halmashauri yetu fedha zikaongezwa mpaka milioni 150 mwaka 2013 na 2014 mpaka milioni 250; mpaka sasa milioni 500 zipo katika mzunguko. 
 9. Zena Hashim (28) mjasiriamali mkazi wa Jangwani
Mabondeni kila kukicha wapiga kura wako tunateseka, wengine hatuju
i mahala pa kwenda, wewe husemi lolote kutusaidia wananchi wa Ubungo Maziwa. Kwa nini?
Jibu: Zena Hashim amejitambulisha kama mkazi wa Jangwani eneo la mabondeni ambalo si sehemu ya Jimbo la Ubungo bali la Ilala. Hata hivyo  tunapaswa kuwa na mipango ya kuhudumia mito katika Jiji la Dar es Salaam kama ambavyo tunafanya kwa barabara ili kujihadhari kabla ya hatari.
10. Godwin Ntogeji( 41), Mkazi Mbezi.
Michango kwa wanafunzi wa shule za misingi imekuwa ni kero kubwa sana kwetu wazazi, je, Mnyika umechukua hatua gani kunusuru hali hiyo?
Jibu: Ni kweli kwamba kuna kero ya michango kwa wanafunzi wa shule ya msingi pamoja na madai ya Serikali kwamba elimu katika ngazi hiyo ni bure.

Kupitia Baraza la Madiwani la Manispaa ya Kinondoni ambalo mbunge ni mjumbe tumeazimia kwamba kuanzia sasa michango iwe inaamuliwa na Mkutano Mkuu wa Wazazi na siyo Kamati au bodi za shule

No comments: