Katibu mkuu wa NCCR MAGEUZI ndugu MOSENA NYAMBABE akizngumza na wanahabari mapema leo kuhusu mchakato wa uchaguzi wa ndani ya chama hicho na utaratibu mzima wa kuchukua form za kuomba nafasi |
Chama cha NCCR MASGEUZI leo kimetangaa rasmi kuanza
mchakato wa uchaguzi ndani ya chama hicho ambapo kimetangaza kuwaruhusu wanachama wa chama hicho kuchukua
form za kuomba nafasi ya kugombea uongozi katika uchaguzi ujao mwishoni mwa
mwaka huu.
Akizungumza na wanahabari mapema leo katibu mkuu wa
chama hicho MOSENA NYAMBABE amesema kuwa utaratibbu wa umoja wa katiba ya wanacnhi
UKAWA ni kuwa kila chama kitateua wagombea wake katika nafasi za
udiwani,ubunge, na urais ambapo baadae watachujwa ili kupatikana wagombea wa
UKAWA katika nafasi hizo
Akitaja ratiba ya uchukuaji wa form ndani ya chama
hicho amesema kuwa kuanzia tarehe 15 hadi 30 mwezi wa tatu wanachama wanaotaka
kuchukua form za udiwani wanaruhusiwa kuchukua form katika ofisi za kata
mbalimbali zilizopo nchi nzima.
Na kuanzia tarehe 20 hadi tarehe 31 mwezi huu wa
tatu wanaotaka kuchukua form za uwakilishi pamoja na ubunge ndani ya chama
hicho wanatakiwa kuchukua form hizo katika ofisi za majimbo,na baadae wagombea
wa nafasi ya uraisi wataanza kuchukua form kuanzia tarehe 1 hadi 30 ya mwezi wa nne kwa
ajili ya kuomba nafasi ya kugombea nafasi hiyo.
Bwana mosena amesema kuwa wao kama chama wanaruhusu
mtu yoyote ambaye ni mwanachama hai wa chama hicho na amekidhi vigezo kuja kuchukua
form hizo hata kama amejiunga jana kwani baadae kutapita mchujo na kama
ikionekana anafaa kukiwakilisha chama hicho jina lake litatua mezani kwa UKAWA
kwa ajili ya mchujo.
Katika hatua nyingine chama hicho kimeeleza
kutokuelewa zoezi alilolifanya RAISI KIKWETE la kubadilisha baadhi ya wakuu wa
wilaya kwa kile alichokiita kuwa hawana kazi ya kufanya Zaidi ya kufanya kazi
za chama tawala na kuwasaidia katika shughuli zao za kisiasa.
Mosena amesema kuwa kazi wanazofanya wakuu wa wilaya
zinaweza kufanywa na wakurugenzi katika wilaya hivyo kuendelea kuwepo ka cheo
hicho ni unyonyaji wa mali za watanzania huku nchi ikiendelea kuwa katika hali
ya umaskini wa kupindukia.
“sisi tunaona ni muendelezo wa ccm na serikali kutengeneza
mtandao wa kukilinda chama hicho kwani hatuoni kazi wanazofanya katika utendeji
wa serikali”alisema mosena.
Aidha amesema kuwa ni kichekesho kuona watu waliochaguliwa kwani hawana sifa za kuwa
katika nafasi hiyo na inaonyesha kuwa ni jinsi gani rais ameidharau nafasi hiyo
na kuamua kuwapa watu ili kuwalipa fadhila.
No comments:
Post a Comment