Friday, February 27, 2015

TIZAMA KAULI YA ZITTO KABWE KUHUSU WAKINA TIBAIJUKA KUPANDISHWA KWENYE KAMATI YA MAADILI



Kazi inayofanyika katika Baraza la Maadili ni kazi nyeti sana ambayo inajenga 'misingi madhubuti ya uwajibikaji' ili kupambana na rushwa kwa viongozi wa umma. Iwapo Baraza hili lingekuwa limeanza kufanya kazi namna hii tangu mwaka 1995 sheria ya Maadili ilipotungwa, (Sheria hii ilitokana na Muswada binafsi wa Mbunge Jenerali Ulimwengu ), angalau tungekuwa tumeondosha 'impunity' iliyokita mizizi nchini kwetu.
Moja ya adhabu kwa mujibu wa Katiba kwa mtu aliyekiuka maadili ya Viongozi wa Umma ni kupoteza nafasi ya Uongozi aliyonayo. Wananchi tushinikize kwamba Tangazo la Mali na Madeni ya Viongozi wa Umma liwe wazi bila masharti ili kwanza kuwaumbua wanaodanganya mali zao na pili kuwaburuza kwenye Baraza la Maadili kueleza wamepataje Mali walizonazo na za wenza wao.
Taasisi za Uwajibikaji zipo, tatizo hazifanyi kazi inavyotakiwa. Sakata la Escrow limeibua taasisi hizi. Tusiishie hapa

No comments: