Mwenyekiti wa ADC Tanzania Bwana SAID MIRAAJ ABDULLA akizngumza na wanahabari leo |
CHAMA cha alliance for democratic change ADC leo kimeitaka
serikali ya Tanzania kuacha kupiga kelele na kufanya mauaji ya walemavu wa ngozi kama mtaji na
badala yake wahakikishe kuwa wanawalinda watanzania wote kwani watanzania wengi
wapo hatarini kutokana na majanga mengi yanayolikumba taifa kwa sasa.
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dare s salaam
mwenyekiti wa ADC Tanzania Bwana SAID MIRAAJ ABDULLA amesema kuwa kuna baadhi
ya watu na viongozi wa serikali wameamua kuyafanya mauaji ya ya walemavu wa
ngozi kama ni mtaji wao wa kujitafutia umaarufu na kuwakandamiza baadhi ya watu
wanaowatuhumu kuhusika na mauaji hayo.
Amesema kuwa kitendo kinachofanya na viongozi wa
serikali cha kuwakamata waganga wa jadi katika baadhi ya mikoa hapa Tanzania
kwa kile wanachowatuhumu ni wauaji wa albino ni udhalilishaji mkubwa kwa
waganga hao ambao wamekuwa msaada wa wananchi katika maeneo ambayo hakuna
hospitali kwani hakuna ushahidi wowote unaoonyesha moja kwa moja kama waganga
hao wanahusika.
“hivi kuna sehemu ina waganga kama
sumbawanga,tanga,na bagamoyo,kwanini huko mauaji ya albino hakuna,au huko
hawajui kama kuna waganga,huu ni udhalilishaji mkubwa kwa hawa waganga,hivi
kwanini kuanza kuwakamata leo na sio toka walipoanza?”alihoji mwenyekiti huyo
wa chama ambacho bado ni kipya nchini Tanzania.
Ameongeza kuwa kwa sasa Tanzania kila mwananchi yupo
katika hatari ya kufa akitolea mfano mauaji ya vikongwe,ajali za barabarani,askari
kuua raia,vifo vya kina mama na watoto,na mauaji yanayofanywa na wananchi wenye
hasira kali,ambapo amesema kuwa serikali inatakiwa kuanza kuyatizama haya kwani
yamekuwa yakiua watanzania wengi zaidi ya hao walemavu wa ngozi.
“Hivi ni watu wangapi wanakufa katika ajali kwa
mwaka nchini Tanzania,hivi ni wakina
mama wangapi wajawazito wanakufa katika mahospitali kwa kukosa matibabu
sahihi,hivi ni watoto wangapi wanakufa katika mahospitali yetu,iweje leo mauaji
ya alibino ndio yaonekane yanaua watu wengi na kufanya watu wasahau mambo
mengine.
Aidha amesema kuwa mauaji ya watu wenye ulemavu wa
ngozi nchini tanzania sasa yamefikia hatua ambayo lazima vyombo ambavyo
vinahusika kusimamia usalama wa raia kuchukua hatua stahiki kudhibiti vitendo
hivyo na sio kuwakamata waganga pekee na kufanya hivyo ni kuonyesha kuwa
serikali imeshindwa kabisa kuwakamata watu ambao wanafanya vitendo hivyo moja
kwa moja.
Amesema kuwa kwa kuonyesha kuwa chama hicho kipi
pamoja na walemavu wa ngozi baadhi ya viongozi wao ni watu wenye ulemavu wa
ngozi ambapo amewataka watanzania kacha imani ambazo zinawafanya wasahau utu wa
mwanadamu na kuua walemavu hao katika maeneo mbalimbali nchini.
No comments:
Post a Comment