TIMU ya Coastal Union imewasilia
jijini Tanga ikiwa na mikakati mizito ya kuhakikisha inawanyamazisha wapinzani
wao Azam FC ikiwa ni muendelezo wa Michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara
mchezo unaotarajiwa kucheza kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani wikiendi ijayo.
Akizungumza leo na waandishi wa habari, Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema
kuwa sasa nguvu zao watazielekeza kwenye mchezo huo utakaochezwa kwenye mjini
hapa.
Amesema kuwa dhamira yake aliyoipanga ni
kuchukua pointi tatu muhimu dhidi ya Ruvu Shooting haikuweza kutimia na
kujikuta wakilazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 hivyo atahakikisha inatimia
kwenye mechi hiyo.
Amesema timu hiyo imerudi
salama mkoani hapa na tayari wameshaanza kujipanga imara kuhakikisha
mechi hiyo timu inapata ushindi n kutokana na uimara wa kikosi chao
Aidha amesema kuwa wachezaji wa
kikosi hicho wameimarika zaidi na wapo imara kuweza kupambana kufa na kupona
ili kuchukua pointi tatu muhimuzo zitawasogeza kwenye nafasi za juu kwenye
msimamo wa Ligi hiyo.
Hata hiyo amewataka wapenzi na
mashabiki wa soka mkoani hapa kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi katika mchezo
huo ili kuipa hamasa timu hiyo kuweza kutimiza ndoto zake.
No comments:
Post a Comment