RUSHWA.
Viongozi wa JUKATA wakiongozwa na kaimu mwenyekiti HEBRON MWAKAGENDA wakizungumza na wanahabari mapema leo |
Wakati serikali kupitia tume ya taifa ya uchaguzi
ikiendelea kurattibu mchakati wa uandikishwaji wa daftari la kidumu la wapiga
kura kwa mfumo wa BVR zoezi ambalo lilianzia katika miji ya njombe,tuhuma za rushwa zimeibuka katika
mchakato huo.
Akiibua tuhuma hiyo kaimu mwenyekiti wa jukwaa la
katiba tanzania JUKATA bwana HEBRON MWAKAGENDA amesema kuwa kumekuwa na vitendo
kadhaa vya rushwa katika zoezi hilo ambapo baadhi ya wananchi wamekuwa wakitoa
rushwa ili kuandikishwa mapema katika zoezi hilo baada ya kusota kwenye foleni
kwa muda mrefu .
Amesema kuwa ktokana na upungufu wa vifaa katika
zoezi hilo ambapo watu zaidi ya 26000walitakiwa kujiandikisha ambapo mashine za
kufanya kazi hiyo zilikuwa 38 tu jambo ambalo lilipelekea usumbufu wa wananchi
na wengine kuamua kususia zoezi hilo.
Ameongeza kuwa utafiti ambao ulifanywa na jukwaa
hilo kuanzia tarehe 18 hadi 22 mwezi wa tatu unaonyesha kuwa hali bado ni tete
na ni kata moja tu ya YAKOBI iliyoonekana kukamilisha zoezi hilo kwa asilimia
80 wakati kata nyingine zikiendelea kusua sua,ambapo amesema hadi sasa wananchi
waliofanikiwa kujiandisha mpaka tarehe 22 mwezi wa tatu kwa kata zote walikuwa
17000 na hivyo wananchi zaidi ya 9000 wamebaki bila kujiandikisha.
Ameongeza kuwa kumekuwa na habari ambazo ni za
kiuaminika kuwa serikali inajiandaa kuendesha zoezi la kura ya maoni kwa
kutumia daftari la kudumu la zamani ambalo kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume ya
taifa ya uchaguzi jaji DAMIANO LUBUVA anasema kuwa daftari hilo limechafuka
sana na halifai kiasi ambacho haliwezi kurekebishika tena.
No comments:
Post a Comment