Jukwaa la katiba tanzania JUKATA wameitaka serikali
kuahirisha mchakato mzima wa upatikanaji wa katiba mpya hadi mara baada ya
uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka huu kwa kile walichodai kuwa ni mchakato huo
kujawa na mapungufu mengi ikiwemo maandalizi mabovu yanayofanyika kuelekea katika upigaji
wa kura ya maoni juu ya katiba pendekezwa.
Akizungumza na wanahabari mapema leo jijini Dar es
salaam kaimu mwenyekiti wa jukwaa hilo ndugu HEBRON MWAKAGENDA amesema kuwa
kusuasa sua kwa zoezi la uandikishwaji wa daftari la kudumu kwa mfumo mpya wa
BVR,ni ishara tosha kuwa ni ndoto kwa Tanzania kupata katiba bora kwani hadi
sasa kuna idadi kubwa ya wananchi ambao hawajajiandikisha katika daftari hilo
huku muda wa kupiga kura hiyo ukiwa unakaribia jambo ambalo limekuwa
likimtatiza kila mtanzania kama jambo hilo linawezekana.
Amesema kuwa kutokana na upungufu wa vifaa pamoja na
rasilimali nyingine unaoonekana wazi katika zoezi hilo ni wazi kuwa daftari
hilo haliwezi kukamilika na kutumika katika kura ya maoni ya katiba.
Amesema kuwa zoezi ambalo lilifanyika katika miji ya
makambako na njombe la uandikishwaji wa daftari hilo limeonekana kuchukua zaidi
ya miezi miwili kukamilika ambapo amehoji kama zoezi hilo linaweza kufanyika
kwa tanzania nzima ndani ya kipindi kifupi ili kufanyika kwa zoezi la upigaji
kura ambao umepangwa kufanyika tarehe 30 mwezi wan ne mwaka huu.
Aidha amesema kuwa kutokana na upungufu huo
unaoonekana kuielemea serikali na kushindwa kuweka wazi kwa watanzania kama
zoezi hilo limeshindikana,JUKATA wanaitaka serikali kuacha mara moja
kuilazimisha tume ta uchaguzi kuendesha zoezi la kura ya maoni kwa njia yoyote
kwani hata mwenyekiti wa tume hiyo amekiri wazi kuwa zoezi hili litakuwa ngumu
kufanyika kwa muda uliopangwa.
Amesema kuwa JUKATA wanaona hakuna umuhimu wala
ulazima wa kulazimisha kupatikana kwa katiba mpya kwa sasa na badala yake
serikali ihamishie nguvu zake katika uchaguzi mkuu wa Tanzania wa mwezi wa kumi
kwani ni uchaguzi wa kihistoria na unahitaji maandalizi ya kutosha kwa wananchi
ikiwemo utoaji wa elimu ya uraia kwa wananchi ili wawezi kuwachagua viongozi
ambao watawasaidia kwa miaka mingine mitano.
Wanahabari mbalimbali kutoka Tanzania wakisikiliza kwa makini |
Katika hatua nyingine JUKATA wamesema kuwa kama
serikali itakuwa kiziwi na kiuendelea na kura ya maoni kwa kutumia daftari la
zamani na hatimaye kupata katiba mpya wao wataanza mara moja harakati za
kuwashawishi wananchi kuingia mitaani kuanza upya kudai katiba mpya nyingine
kwani itakayopatikana itakuwa sio katiba kwa ajili ya watanzania wote.
No comments:
Post a Comment