Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imewasili salama leo
asubuhi jijini Mwanza, tayari kwa maandalizi ya mchezo wa kirafiki wa Kimataifa
siku ya jumapili Machi 29, 2015 dhidi ya timu ya Taifa ya Malawi (The Flames),
mechi itakayochezwa kwenye dimba la Uwanja wa CCM Kirumba.
Kikosi cha Stars kimeondoka kikiwa na wachezaji 18 ambao
wameripoti kambini jana, huku kiugo mshambuliaji Mwinyi Kazimoto anayecheza
soka la kulipwa nchini Qatar akitarajiwa kuungana na wenzake leo mchana jijini
Mwanza.
Wachezaji waliopo kambini jijini Mwanza ni, magolikipa Aishi
Manula na Mwadini Ali (Azam FC), walinzi ni Erasto Nyoni, Shomary Kapombe,
Aggrey Morris (Azam FC) , Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Haji Mwinyi (KMKM),
Hassan Isihaka na Abdi Banda (Simba SC)
Wengine ni Amri Kiemba, Frank Domayo, Salum Abubakar (Azam
FC), Said Ndemla (Simba SC), Haroun Chanongo (Stand United), John Bocco (Azam
FC), Juma Luizio (Zesco United), Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu (TP
Mazembe).
Mchezaji Mcha Khamis wa Azam FC amejiondoa kikosini kutokana
na kuwa majeruhi, huku wachezaji wa Young Africans wakitarajiwa kujiunga na
kikosi hicho cha timu ya Taifa mara tu baada ya mchezo wao wa Ligi Kuu ya
Vodacom dhidi ya JKT Ruvu siku ya jumatano.
MALAWI
KUWASILI ALHAMISI
Msafara wa watu 25 wa timu ya Taifa ya Malawi (The Flames) unatarajiwa
kuwasili jijini Dar es salaam siku ya alhamis, kabla ya kuunganisha ndege siku
ya ijumaa kuelekea jijini Mwanza tayari kwa mchezo wa kirafiki wa kimataifa
dhidi ya Taifa Stars siku ya jumapili.
Katika msafara huo utakaokuwa na wachezaji 18 na viongozi 7,
kocha mkuu wa The Flames Young Chimodzi amewajumuisha wachezaji nane (8) katika
kikosi chake wanaocheza soka la kulipwa katika nchi za Afrika Kusini, Congo DR,
Msumbuji na Zimbabwe.
Wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini ni
Limbikani Mzava (Celtic), Harry Nyirenda (Black Leopards), Esau Kanyenda
(Polokwane City), na Atusaye Nyondo (University of Pretoria).
Wengine ni Nahodha Joseph Kamwendo (Tp Mazembe - Congo DR),
Frank Banda (HBC Songo - Msumbuji), Chimango Kayira (Costal De Sol - Msumbuji)
na Gerald Phiri (Caps United - Zimbambwe).
VPL
KUENDELEA KESHO
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ianatrajiwa kuendelea
kesho (jumatano) kwa mchezo mmoja kupigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam, kwa wenyeji JKT Ruvu kuwakaribisha vinara wa ligi hiyo timu ya Young
Africans.
KILUVYA
BINGWA SDL
Timu ya Kiluvya United ya mkoa wa Pwani jana imetawazwa
Mabingwa wapya wa Ligi Daraja la Pili (SDL) baada ya kuifunga Mbao FC ya Mwanza
kwa mabao 4-2 katika mchezo wa fainali uliofanyika kwenye Uwanja wa kumbukumbu
ya Karume jijini Dar es salaam.
Kiluvya United inaunganana timu za Mji Mkuu (CDA) ya
Dodoma, Mbao FC ya Mwanza na Mji Njombe ya Njombe kupanda Ligi Daraja la Kwanza
(FDL)msimu ujao, huku timu za Ujenzi Rukwa, Katavi FC na Volcano zikishuka
daraja kutoka Ligi Daraja la Pili.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment