Chama cha wananchi CUF
leo kimemtaka Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk JAKAYA KIKWETE pamoja
na tume ya uchaguzi nchini kukiri mbele ya wananchi kuwa hakuna uwezekano wa
kufanyika kwa kura ya maoni juu ya katiba pendekezwa kwa kile wanachodai ni
kushindwa kukamilisha uandikishwaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa
wakati.
Akizungumza na
wanahabari leo makao makuu ya chama hicho jijini Dar es salaam naibu mkurugenzi
wa habari na uenezi wa chama hicho ABDUAL KAMBAYA amesema kuwa CUF wanaitaka
tume ya taifa ya uchaguzi itamke kushindwa na kutokuwepo kwa uwezekano wa kuwepo
kwa kura ya maoni ili kuepusha taifa kuingia gharama za kutumia fedha nyingi
kuandaa kura ya maoni wakati zoezi lenyewe linaweza lisiwepo kwani ukamilifu wa
uandikishwaji wa daftari la kudumu kwa mfumo wa BVR hauwezekani tena kwa tarehe
iliyopangwa.
Amesema kuwa mbali na
mazingira halisi ambayo yanaonyesha kuwa zoezi hilo limekwama na halitawezekana
serikali imekuwa ikilazimisha kwamba inawezekana akitolea mfano kauli ya waziri
mkuu aliyoitoa kuwa kura ya maoni iko pale pale na uandikishwaji utamalizika kwa
wakati,hali ambayo amesema kuwa inaashiria hali isiyo njema kwa serikali ya CCM
kuhusu hatma ya usala wa nchi wakati wa zoezi la kura ya maoni.
Amesema kuwa kuna mambo
kadhaa ambayo yanafanya zoezi la BVR lisikamilike ikiwemo idadi kubwa ya watu
wanaojitokeza ukilinganisha na vifaa husika,uwezo mdogo wa mashine hizo kufanya
kazi,idadi ndogo ya madhine hizo,pamoja na serikali kutokuwa na hela ya kutosha
kuendesha zoezi hilo kwa sasa,ambapo amesma kuwa hakuna muujiza wowote unaoweza
kutokea katika zoezi hilo.
Akizungumzia kauli
aliyoitoa Raisi KIKWETE na kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akivitaka
vyombo vya ulinzi na usalama ikiwemo polisi kujiandaa kwa ajili ya zoezi la
kura ya maoni,amsemaji huyo wa CUF amesema kuwa kauli hiyo ni kauli ya vitisho
na kuashiria utawala wa mabavu na kusema kuwa huu sio muda wa mabavu ni muda wa
kutafakari na kufanya maamuzi sahihi ambayo yatakuwa na manufaa kwa watanzania
wote.
SOMA TAMKO NZIMA HAPO CHINI
No comments:
Post a Comment