Monday, March 2, 2015

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI KUAGA MWILI WA MAREHEMU KAPTEN KOMBA VIWANJA VYA KARIMJEE DAR LEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakeze Mama Zakhia Bilal na Mama Asha Bilal, wakitoa heshima zao za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Kapteni John Komba, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika leo Machi 2, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Baada ya shughuli hiyo mwili wa marehemu umesafirishwa kuelekea Kijiji cha Litui Wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma kwa maziko. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, wakati walipokutana kwenye Viwanja vya Karimjee baada ya kuhudhuria shughuli za kuaga mwili wa marehemu Kapteni John Komba leo Machi 2, 2015. Baada ya shughuli hiyo mwili wa marehemu umesafirishwa kuelekea Jijini cha Litui Wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma kwa maziko. Picha na OMR

No comments: