Ikiwa bado sakata la
kufukuzwa uanachama kwa mbunge wa kigoma kaskazini (CHADEMA) mh ZITTO KABWE
linaendelea kuchukua nafasi katika vichwa vya watanzania na wapenda siasa,mbunge huyo
ameanza kufanya ziara ya siku tatu jimboni kwake kuzungumza na watanzania
mbalimbali.
Akiwa katika ziara yake MBUNGE
wa Kigoma Kaskazini,Zitto Kabwe(Chadema),amewataka wakazi wa mkoa wa kigoma
wasisikitishwe na mambo yanayomkabili kwa sasa kwa kile alichoeleza kuwa
asilimia kubwa ya wanasiasa makini walishapitia misuko suko kama yake.
Amewaeleza kuwa jambo la msingi ni
kumuunga mkono katika hatua yoyote atakayochukua kwa ajili ya wanakigoma na
Taifa kwa ujumla katika kumaliza mgogoro uliopo baina ya Chama chake na yeye
Zitto ametoa kauli
hiyo leo mjini Kigoma alipokutana na viongozi 250 kwenye mkutano wa ndani
uliohusisha viongozi kutoka katika kila kijiji kwenye jimbo la Kigoma
kaskazini yenye jumla ya vijiji 45.
Aliwataja baadhi
ya wanasiasa waliopita katika hatua kama yake na baadae wakageuka
washindi kuwa ni Maalim Seif Sharif Hamad(Tanzania),Mahathir Mohamed(Malaysia
na Indira Gandhi wa India.
“Msinililie mimi kwa kuwa haya ni
mapito ya kila mwanasiasa Makini,wengi walio makini walitofautiana na vyama
vyao kwa sababu ya maslahi ya mataifa yao,wapo walioanzisha vyama baada ya hali
hiyo na wakashinda na wapo waliopigiwa magoti na vyama vyao baada ya kugundua
walichofanya si sahihi, hivyo jukumu kubwa ni kuniunga Mkono”alisema Zitto.
Alisema mpaka sasa hajapewa taarifa
yoyote ya kusitishwa kwa Ubunge wake na kama hali hiyo ikijitokeza atarudi
kuwafahamisha juu ya hatua atakayochukua.
Zitto yupo mjini Kigoma kwa ziara
ya siku tatu,ambapo atawatembelea wakulima wa mradi wa Kahawa walio katika
mfuko wa hifadhi ya Jamii(NSSF), pamoja na kukabidhi gari aina ya Ambulance
katika kituo cha Afya Nyarubanda na kisha kufanya mikutano miwili ya hadhara.
Juzi Mwanasheria mkuu wa Chadema
Tundu Lissu,alitangaza hadharani kuvuliwa uanachama kwa Zitto kutokana na
kushindwa katika kesi aliyofungua kupinga asijadiliwe na Chama Chake
PICHA JUU NI YA MAKTABA,TUNAENDELEA KUTAFUTA PICHA HALISI ZA ZIARA
|
No comments:
Post a Comment