STORY NA IZACK MAGESA
BALAZA la madiwani
Halamshauri ya Temeke wamemtaka Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kuhakikisha
anatenga bajeti maalumu ili kunusuru jamii pindi ianapokumbwa na maafa mbali
mbali.
Hayo yalisemwa Dar es
salaam leo,wakati wa Balaza hilo lilikutana kujadili mambo mbali mbali
yanayowahusu ikiwa ni moja ya mchakato wa kukuza maendeleo wilayani Temeke.
Akizungumza na Waandishi
wa habari Dar es salaam leo.,Diwani wa kata ya Keko Francis Mtawa alisema
lazima ifikie mahala Halmshauri iweze kutenga bajeti maalumu ya mahafa badala
ya kutenga kitengo cha mahafa ambacho kipo chini ya ofisi ya Waziri Mkuu
Bw Mizengo Pinda.
"lazima ifikie
mahala na sisi kama Halmashauri iwe na bajeti ya mahafa badala ya kutegemea
kitengo cha mahafa kilichopo Ofisi ya Waziri Mkuu,ambapo inakuchukua muda sana
mpaka kuja kufikiwa 'alisema.
Madiwani mbalimbali kutoka manispaa ya temeke wakiwa wanaendelea na mkutano huo uliofanyika leo |
No comments:
Post a Comment