Friday, March 6, 2015

RAIS KIKWETE AULIZA HAPA NI TANZANIA AU ULAYA,STUDIO ZA AZAM TV ZAMDUWAZA




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akifunua jiwe la msingi la jengo la Azam TV, Tabata Relini, Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa studio za kisasa kampuni hiyo.
Rais kikwete akizngumza baada ya kuzindua rasmi studia hizo
RAIS Jakaya Kikwete leo ameshindwa kujiuzuia baada ya kutoa mshangao wake baada ya kuona ubora wa Studio za kisasa za kurushia Matangazo  ya Kituo cha Azam TV   ambazo zinalingana na Runinga Bora Duniani kama  vile CCN,BBC,Al-Jazeera,DW,Anaandika KAROLI VINSENT Endelea nayo
    
Azam tv ambayo inamilikiwa na Mfanyabiashara Maarufu Nchini Said Salim Bakhresa wamejenga Studio hizo ambazo zipo Tabata Relini Jijini Dar es salaam zenye Thamani ya pesa za kitanzania Zaidi ya bilioni 56.

Akizindua Studio hizo Bora za kisasa Kabisa kuwepo Kusini mwa Jangwa La Sahala leo, Rais Jakaya Kikwete Amemwagia sifa Mfanyabiashara huyo na kusema ameleta  mapinduzi makubwa katika sekta ya Habari nchini na kuwataka wamiliki wengine wa Runinga nchini kuiga mfano na Mfanyabiashara huyo.
     
 Kuzinduliwa huko kwa Studiao hizo za kisasa,kunakuja ikiwa Kampuni hiyo ya Azam tayari imeshapata Leseni ya kurusha Moja kwa Moja mechi ya Ligi kuu ya Vodacom ya Tanzania Bara,na pia wako mbioni kuonyesha pia Ligi kuu mbalimbaliza Soka Afrika Mashariki na sasa ameshapiga hodi nchini Uganda.
      
Mbali na Runinga Mfanyabiashara huyo pia ameanzisha  Radio yake hapa jijini.
Wafanyakazi wanena.

Wafanyakazi mbalimbali wa Runinga ya Azam waliozungumza na mwandishi wa Mtandao huu kwa Sharti ya kutotaja majina yao mtandaoni, wamemwagia sifa Mfanyabiashara huyo na kusema ni Mmiliki pekee nchini, wa Vyombo vya Habari anayelipa vizuri.
   
     ‘Sikifuchi mimi nimefanya kazi kwenye Vyombo mbalimbali nchini kusema kweli kwa sasa nilivyohamia hapa Azam Media huyu mmiliki wetu anatujali sana kwanzia vitendea kazi na pia malipo mazuri”

Wimbi la watangazaji nchini kuhamia Azam media.
Taarifa za Kuaminika ambazo mtandao huu umezipata unasema kwa sasa Mfanyabiashara huyo ameweka mipango ya ,kuwachukua watangazaji mbalimbali kutoka Redio na televisheni kuja kuhamia kwenye Redio yake mpya.


Kaimu mkurugenzi wa azam media TIDO MHANDO
Mkurugenzi Mkuu wa Azam Media Limited, Yussuf Bakhresa katika hafla hiyo  






No comments: