Tuesday, March 17, 2015

UKWELI KUHUSU BONDIA CHEKA KUACHIWA HURU LEO HUU HAPA

Unakumbuka ile skendo iliyompata bondia wa ngumi nchini Francis Cheka baada ya kumpiga na kumuumiza meneja wa baa yake akimtuhumu kusababisha hasara?

Taarifa iliyotolewa na kocha wake Abdalah Komando na kuthibitishwa na wanafamilia yake inasema Bondia huyo nyota zaidi nchini sasa ameachiwa huru na atakuwa akitumikia kifungo cha nje.
Alisema Cheka ameachiwa huru baada ya kushinda rufaa yake aliyokata kupinga kifungo cha miaka mitatu gerezani na sasa anatumikia kifungo cha nje.
Tayari Cheka alianza kutumikia kifungo hicho mjini Morogoro lakini taarifa za uhakika zinasema ameachiwa leo baada ya kushinda rufaa hiyo.
“Tayari ameachiwa, Ila tayari yuko nje, tunashukuru kwa hatua hii lakini bado kesi yake inaendelea kwa kipindi chote cha miaka mitatu” alisema kocha wake Abdalah Komando
Cheka alihukumiwa kwenda jela baada ya kumuumiza meneja wa baa yake mjini Morogoro akimtuhumu kumsababishia hasara katika baa yake.

No comments: