Akizungumza na na waandishi wa habari leo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Yanga Jerry Muro amesema wameshangazwa na mabadiliko ya kila kukicha ya ratiba ya ligi hasa mchezo wao dhidi ya JKT Ruvu ambao walitakiwa waucheze kesho kwa mujibu wa ratiba yao.
Muro amesema bodi ya ligi imeonyesha kwamba haitaki Yanga ifanikiwe katika kampeni zao za kombe la Shirikisho kwa kuitaka kuucheza mchezo huo Machi 11 ikiwa ni siku tatu kabla ya kushuka katika Uwanja wa Taifa kucheza na Plutinum ya Zimbabwe.
"Ratiba tuliyonao inayonyesha kwamba kesho kulitakiwa tucheze dhidi ya JKT Ruvu lakini hawa wenzetu kwa matakwa yao wamebadilisha ratiba pasipo kutuhusisha hii kwetu tunaichukulia kama hujuma,"amesema Muro.
"Tumewaambia tangu jana kama wameufuta mchezo wa kesho na badala yake wakaupeleka Machi 11 Yanga hatutakuja uwanjani kwakuwa huo sio uzalendo hatuwezi kuacha maandalizi ya mechi yetu ya kimataifa kuangalia mechi ya ligi.
No comments:
Post a Comment