Baraza kuu la uongozi
la taifa ndani ya chama cha wananchi CUF limemtaka Rais wa wajamhuri ya muungano wa Tanzania Dk JAKAYA KIKWETE
kukaa kwa pamoja na wadau wa uchaguzi nchini hususani vyama vya siasa kujadili
kwa pamoja hali ya uandikishwaji wa daftari la ludumu la wapiga kura kutokana
na sintofahamu inayoendelea nchini.
Akisoma maadhimio ya
baraza hilio lililokaa kwa siku mbili
jijini Dar es salaam mwenyekiti wa chama hicho profesa IBRAHIMU LIPUMBA amesema kuwa baraza hilo
limesikitishwa sana na kasi ndogo ya uandikishwaji wa daftari la kudumu la
wapiga kura kwa mfumo wa BVR ambapo mpaka sasa tume haijamaliza zoezi hilo kwa
mkoa mmoja wa njombe jambo ambalo amesema sio ishara nzuri kuelekea uchaguzi
mkuu Mwaka huu..
Amesema hali iliyopo sasa
inaonyesha ishara mbaya hali inayoweza kusababisha kuahirishwa kwa uchaguzi
mkuu ujao kwa sababu hali ya vifaa vya uandikishaji bado ni ndogo na hakuna
jitihada za makusudi za kurekebisha hali hiyo.
Ameongeza kuwa tume ya
taifa ya uchaguzi ilianzisha mchakato huo bila kutengewa fedha za kutosha za
kununulia vifaa kuajiri na kuwapa mafunzo wafanyakazi watakaotumia mashine
hizo,pamoja na kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa zoezi hilo hali
ambayo imeathiri mchakato huo kwa kiasi k,ikubwa.
Aidha amesema kuwa huu
sio muda wa kuzidi kutupiana mpira bali sasa ni muda wa raisi KIKWETE kuingilia
kati zoezi hilo na kukubali kuwasikiliza wadau mbalimbali wa uchaguzi ili kwa
pamoja washauriane nini cha kufanya ili uchaguzi mkuu uwepo katika tarehe
iliyopangwa.
Katika hatua nyingine
baraza hilo limeunga mkono maadhimio ya umoja wa katiba ya wananchi UKAWA ya
kutoshiriki katika kura ya maoni juu ya katiba pendekezwa kwa kile walichoita
kuwa haina maoni ya wananchi na haina faida kwa mtanzania wa kawaida.
|
No comments:
Post a Comment