Diwani wa kata ya kijiji Mh ANDERSON CHALLE akipiga mpira wa penalt kama ishara ya kuzindua rasmi mashindano hayo jana katika viwanja vya suhle ya msingi kijichi Jijini Dar es salaam |
Diwani wa kata ya Kiijichi kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Mh ANDERSON CHALE amezindua
rasmi mashindano ya mpira wa miguu katika kata yake ambayo anayafadhili
mashindani yatakayoshirikisha timu 60 kutoka katika kata hiyo mashindano ambayo
yamepewa jina la UVCCM KIJICHI CUP
Akizindua mashindano
hayo jana jijini Dar es salaam diwani huyo amesema kuwa mashindano hayo yana
lengo la kuwakusanya vijana na wananchi wa kata hiyo kwa pamoja ili kujenga
umoja wa pamoja katika kuendesha shughuli mbalimbali za kimaendeleo katika kata
hiyo.
Mashindano hayo ambayo
ni mara ya nne kufanyika na kudhaminiwa na Diwani huyo yanatarajiwa kugharimu
zaidi ya Million 35 hadi kumalizika kwake ambapo diwani huyo amesema kuwa
anafanya hivyo kutokana na nafasi yake aliyonayo kama Diwani ya kuwaleta
wananchi pamoja na kujenga ushirikiano katika Kata hiyo.
Akizungumza na mtandao
huu baada ya kufanya uzinduzi wa mashindano hayo ambao ulifanyika katika
viwanja vya shule ya msingi kijichi Diwani CHALLE amesema kuwa lengo lake lingine
ni kuona kuwa anakamilisha miradi mbalimbali ambayo amejiwekea katika kata hiyo
ikiwemo ya maji,barabara na miradi mingine mingi ya kimaendeleo ambayo tayari
ameianza ambapo ametumia nafasi hiyo kutangaza nia yake ya kugombea tena nafasi
hiyo katika uchaguzi wa mwaka huu ili kupata nafasi ya kuongoza kwa miaka
mitano mingine aweze kumaliza kile ambacho alikianza.
Amewataka Wananchi
kuendelea kumwamini na ikizingatia kuwa hii ni awamu yake ya kwanza kuiongoza
kata hiyo ambapo amesisitiza kuwa anahitaji nafasi zaidi ya kuendelea kuongoza
kata hiyo ili kuhakikisha kuwa anafikia malengo aliyojiwekea wakati anatafuta
nafasi ya kuwatumikia wananchi hao.
Viongozi mbalimbali wa chama cha mapinduzi katika kata hiyo wakiongozwa na diwani wao Mh ANDERSON CHALLE wakishugudia moja kati ya michezo ya ufunguzi wa mashindano hayo |
No comments:
Post a Comment