Friday, April 24, 2015

VIDEO--KAZI IPOI--MBOWE NAYE APEWA UCHIEF AITWA MAYEGO-TIZAMA TASWAIRA MBALIMBALI KATIKA ZIARA ZAKE

Wazee wa kabila la wasukuma wakimuombea kwa Mwenyezi Mungu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, ili yeye na chama chake aweze kutawala nchi. Mbowe alisimikwa na kupewa zana za kitemi za kabila hilo na kuitwa jina la Mayego kabla ya kuanza kuhutubia mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Kijiji cha Lagangabilili wilayani Itilima mkoani Simiyu


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Lagangabilili Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu juzi.
Mamia ya wananchi wa Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, wakimshangilia Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe (hayupo pichani), katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Lagangabilili wilayani humo
Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakipasha mwili kwa kurukaruka mbele ya Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe (hayupo pichani), katika Kambi ya mafunzo ya kujenga mwili, afya, ujasiliamali, uzalendo na kulinda kura na mali za umma, iliyopo Luhemeli Kata ya Ndala Wilaya ya Nzega mkoani Tabora juzi. Mbowe aliyafunga mafunzo hayo baada ya vijana hao kukaa kambini kwa siku tatu.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe (wa tatu kulia), akiongoza halaiki ya vijana, viongozi na makada wa chama hicho kukimbia mchakamchaka kutoka kwenye Kambi ya mafunzo ya vijana ya Luhemeli Kata ya Ndala wilayani Nzega Mkoa wa Tabora, kuelekea kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Taifa-Ndala

No comments: