Mwenyekiti wa chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA mh FREMAN MBOWE akiwasili katika viwanja vya PTA sabasaba jijini Dar es salaam kwa ajili ya ufunguzi wa mafunzo hayo maalum |
Mwenyekiti wa chama
kikuu cha upinzani nchini Tanzania CHADEMA Mh FREMAN MBOWE leo amezindua rasmi program
maalum ndani ya chama hicho ya mafunzio kwa viongozi mbalimbali wa kanda ya Dar
es salaam mafunzo ambayo yamelenga katika kuwajengea uwezo zaidi viongozi wa
chama hicho na wale wanaotarajia kuwa viongozi baada ya uchaguzi ujao mwishoni
mwa mwaka huu.
Akizindua mafunzo hayo
jijini Dar es salaam leo mh FREMAN MBOWE ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa
umoja wa katiba UKAWA amesema kuwa lengo
kuwa mafunzo hayo yameanzia katika mkoa wa Dar es salaam kwa kuwa ni ukweli
usiopingika kuwa Mkoa huo ndio unaongoza kwa idadi kubwa ya wapiga kura nchini
kwa takwimu za serikali ambapo wameona ni vizuri kuanzia katika mkoa huo na
baadae kueneoa katika maeneo mengine.
Amesema kuwa malengo
makuu ya mafunzo hayo ni kuwajenga viongozi bora, wenye weledi, wanaojua
kuwatumikia wananchi waliowachagua,ambapo amesema mafunzo hayo yatatumika kama
dira kuu ya chama hicho katika kuelekea kile alichokiita ushindi wa kishindo wa
upinzani nchini katika uchaguzi ujao mwaka huu.
Amesema moja kati ya
maazimio makubwa ya mafunzo hayo ni kuwajenga viongozi ambao watakwenda
kushinda nafasi zote za uongozi katika majimbo manane ya mkoa wa dare s salaam
na kufanyika hivyo kwa mikoa mingine nchinio Tanzania.
Umati mkubwa wa viongozi wa CHADEMA kutoka maeneo yote ya Dae es salaam waliohudhuria hapa |
Akizngumza na mamia ya
viongozi mbalimbali na watangaza nia waliojitokeza katika uzinduzi huo amesema
kuwa lengo kuu la UKAWA sio kugawana
nafasi za uongozi kama inavyoendezwa bali ni kuwakomboa watanzania kutoka
katika mikono ya wanyonyaji hivyo akawataka viongozi hao kuacha kufikiri sana
kuhusu nafasi za uongozi bali wafikiri sana katika kuwakomboa wananchi
Mh MBOWE akizungumza |
Aidha amesema kuwa
baada ya kukamilika kwa mafunzo ndani ya mkoa wa dare s salaam viongozi na
wakufunzi wa chama hicho watasambaa nchi nzima katika kueneza mafunzo hayo
ambayo amesema kuwa kila kanda na kila sehemu magfunzo hayo yatafika lengo
likiwa ni kujiandaa kuwa na sertikali bora ifikapo mwezi wa kumi.
Mwenyekiti MBOWE akizindua vitabu ambavyo vitatumika katika mafunzo hayo |
Katika hatua nyingine
akizngumzia umoja wa katiba ya wananchi UKAWA amesema kuwa ni muda wa wanachama
wa vyama hivyo kuwa na matumaini mapya na kuwa na moyo wa subira kwani viongozi
wakuu wa vyama hivyo wanaendelea vizuri na vikao vya kukamilisha makubaliano
yao kabla ya kuja na maazimio na majina ya wagombea wao ambapo amesema kuwa
wale ambao wamekuwa wakisubiri wagombane waendelee kusubiri kwani umoja huo upo
imara kulikp watu wanavyodhani.
TUNAOMBA RADHI KWA UONEKANI HAFIFU WA PICHA ZETU
No comments:
Post a Comment