Madiwani wa manispaa ya Temeke leo wamekagua miradi
mbalimbali ya kimaendeleo na kijamii inayoendelea katika manispaa hiyo ikiwemo
maabara,madarasa na nyumba za walimu.
Akizungumza na wanahabari diwani wa kata ya somangira
AISHA MPINJILA amesema kuwa kukamilishwa kwa miradi hiyo kwa asilimia 99
kutasaidia kuinua kiwango cha elimu katika manispaa hiyo na kwa nchi kwa
ujumla.
Aidha kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Temeke WAZIRI
KOMBO amewataka wanafunzi katika manispaa hiyo kuchagua michepuo ya sayansi
kwani ndio mchepuo wenye suluhisho la ajira kwa sasa nchini huku akiwataka
wanafunzi na walimu kutunza miradi hiyo. Baadhi ya shule ambazo zimetembelewa ni Pemba mnanz secondary,nguva secondary,kidete secondary,kimbiji secondary
No comments:
Post a Comment