Zitto akiwahutubia wananchi Manyoni Mjini |
Mkazi wa Manyoni Mjini Mzee ambaye jinalake halikupatikana
maramoja akichukua picha za video kwa kutumia simu mkutano wa ACT-Wazalendo.
|
CHAMA cha ACT-Wazalendo kimesema
kinaweza kuunganisha nguvu na yama vingine vya upinzani ili kukiondoa chama cha
mapinduzi kwenye uchaguzi mkuu ujao ambapo alisema shauku kubwa ya wananchi ni
kutaka kujua msimamo wa ACT Wazalendo katika kushirikiana na vyama vingine vya
siasa ili kufanikisha malengo ya kuiondoa CCM katika madaraka.
Kauli hiyo ilitolewa LEO mjini
Singida na Kiongozi wa ACT wazalendo Zitto Kabwe wakati akihutubia mamia ya
wananchi katika uwanja wa shule ya msingi ukombozi.
"Tumedhamiria kuleta mapinduzi ya kiuchumi kwa kuubomoa mfumo
unaonyonya wananchi. Msimamo wetu upo wazi na tumeueleza mara
kadhaa"alisema na kuongeza
“ACT- Wazalendo tunaunga mkono juhudi zozote za kushirikiana kwa
vyama na hili linathibitishwa na jina letu Alliance na msimamo wetu kuhusu
mabadiliko ya Katiba. Kubwa tunataka ushirikiano utakaonufaisha wananchi na sio
ushirikiano wa kugawana nafasi za uongozi,” alisema Zitto.
Wakazi wa Mji wa Singida wakishangilia viongozi wa Chama cha
ACT-Wazalendo wakati waa mkutano huo jijini humo leo.
|
Kiongozi huyo wa ACT alisema chama hicho hakina tatizo na kipo
tayari kushirikiana na chama chochote kilichokuwa tayari kushirikiana nao
ikiwemo Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa),
Alisema umoja huo ni lazima uwe na malengo ya kujenga uchumi
shirikishi wenye kuzalisha ajira nyingi na bora, wenye mfumo wa hifadhi ya
jamii kwa wananchi wote na wenye kutokomeza umasikini.
Alikanusha chama hicho kutoa kauli yeyote dhidi ya UKAWA
kama inavyoaminishwa na baadhi ya watu, bali wameweka wazi kuwa lazima misingi
ya kiitikadi na kifalsafa izingatiwe katika ushirikiano wowote
"Tupo tayari kwa umoja kwani ni moja ya misingi mikuu 10 ya
chama chetu na umoja ni nguvu,” alisema Zitto.
Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, akisalimiana na mzee
ambaye alitumia muda mwingi kuwapiga picha za ideo viongozi hao wakiwa kwenye
mkutano Manyoni mjini.
|
Akizungumzia hali ya umaskini kwa mkoa wa Singida, Zitto alisema
pamoja na hali ya umaskini Serikali ya CCM, imeshindwa kupunguza umasikini,
nchini kwa kiasi kikubwa na kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Alisema ripoti ya maendeleo ya binadamu imeonyesha kuwa Tanzania
imeshuka kufikia daraja la chini la nchi zenye kiwango kidogo zaidi cha
maendeleo ya binadamu.
“Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya UNDP kuhusu Maendeleo ya Binadamu
duniani ya mwaka 2014 ambayo imeiweka Tanzania katika kundi la nchi zenye
maendeleo ya binadamu ya kiwango cha chini. Lakini kinachoshitusha ni
kushuka kwa nafasi saba zaidi katika Kipimo cha maendeleo ya binaadamu, (HDI),
ukilinganisha na mwaka 2013.
“Ushahidi mzuri wa jambo hili ni ule unaotolewa na kipimo cha
Maendeleo ya Binadamu (HDI), ambacho hupima maendeleo ya binadamu katika nchi
kwa kuzingatia mkusanyiko wa vigezo vya umri wa kuishi, elimu na kipato,” alisema
Zitto
Zitto akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kintintu mara baada ya
kuzindua tawi la chama hicho
|
Viongozi wa ACT -Wazalendo wakishangilia na wananchi wa wilayani
Manyoni baada ya kuzindua tawi la Manyoni Mjini.
|
Amesema katika ngazi ya mikoa, ripoti hiyo inaonyesha
tofauti kubwa ya viwango vya maendeleo ya binadamu ndani ya Tanzania.
Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Dar es Salaam, Iringa, Ruvuma,
Mbeya, na Tanga ndiyo mikoa yenye kiwango cha juu cha maendeleo ya binadamu.
“Singida inazalisha alizeti na sasa hivi tunajua kwamba watu
wanaojali afya zao, wanapenda kula mafuta ya alizeti na ukiongelea mafuta ya
alizeti, basi yale yaliyo bora yanatokana katika mkoa huu. Lakini pamoja na
fursa hiyo ambayo inaweza kuitumia ili kuinua hali ya maisha ya wananchi,”
alisema
Alisema Mkoa wa Singida una madini lakini jambo la kushangaza bado
umekuwa mkoa wa kwanza kwa umaskini huku madini hayo yakishindwa kuwanufaisha
wananchi hasa wanaozunguka vijiji vya Sambaru na Londoni.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Anna Mghwira,
alisema sasa umefika wakati ni lazima nchi iwe huru kwa kuwa na misingi
imara itakayoimarisha demokrasia nchini.
“Rais aitishe Bunge maalumu ili kufanya marekebisho madogo ya
Katiba kuruhusu uchaguzi huru na wa haki lakini pia Wajumbe wa Tume waombe kazi
na wawe wataalamu.
Alisema ACT inashauri kuitishwa kwa Bunge Maalumu ni kutokana
Bunge la sasa la 10 lina uhai wa mkutano mmoja kabla ya kuvunjwa.
“… hivyo Katibu wa Bunge atangaze nafasi za wajumbe wa Tume,
kamati ya Bunge ya Katiba Sheria na Utawala itafanya mahojiano ya wazi na
kupata majina 22 yatakayopelekwa bungeni,” alisema Anna.PICHA ZOTE ZA MKUTANO ZIPO CHINI
Zitto akisalimiana na wakazi wa Manyoni Mjini |
Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe na Mwenyekiti wa
Chama hicho Anna Mghwira wakizindua tawi la chama hicho kwenye Kijiji cha
Kintintu wilayani Manyoni mkoani Singida.
|
No comments:
Post a Comment