Mbunge wa Vunjo (TLP), Augustine Mrema akiongoza maandamano ya wakazi wa Kijiji cha Lole, Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara ikiwa ni sghemeu ya ziara yake jimboni humo juzi. |
Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema akiwa na wanachama wapya wa chama hicho waliotoka NCCR-Mageuzi, CCM na Chadema mara bada ya kuwakabidhi kadi mpya mara baada ya mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Kata ya Makuyuni, Himo mkoani Kilimanjaro, juzi. |
Aliyekuwa Diwani wa Kata Mwika Kusini (TLP), kabla ya kutimuliwa kwa madai ya kukisaliti chama hicho Meja Jesse Makundi akizungumza kuhusiana na tuhuma zinazomkabili wakati wa mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Lole, jimboni Vunjo mkoani Kilimanjaro juzi. |
Aliyekuwa Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Kata ya Makuyuni, Badi Mandali akizungumza mara baada ya kukabidhiwa kadi ya uanachama wa Tanzania Labour Party (TLP) katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Kata ya Makuyuni, Himo mkoani Kilimanjaro, juzi. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa chama hicho, Augustine Mrema na mkewe Rose Mrema. |
Wanafunzi wa shiul;e ya sekondari Muungano wakimpokea Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema mara baada ya kuwasili shuleni hapo, Himo Mkoani Kilimanjaro, juzi. |
Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema akishiriki katika ujenzi wa bweni la wanafunzi katika Shule ya Wasichana Wenye Vipaji Maalum ya Muungano, Himo Mkoani Kilimanjaro, juzi. |
No comments:
Post a Comment