Mwenyekiti wa chama cha
kisiasa nchini Tanzania cha TLP amesema kuwa afya yake kwa sasa ni imara kwa
ajili ya mapambano ya uchaguzi ujao nchini huku akiwataka watu wanaoendesha
propaganda kuwa afya yake imedhoofika wanyamaze kwani maneno hayo hayana ukweli
wa naina yoyote.
Mwenyekiti huyo ambaye
ni mbunge pekee wa chama hicho kupitia jimbo la vunjo mkoani Kilimanjaro leo
ameendesha matembezi ya kuanzia kuliko na makao makuu ya chama hicho magomeni
jijini Dar es salaam hadi sinza ambapo kumefanyika mkutano mkuu wa mwaka wa
chama hicho,amesema kuwa ameamua kufanya matembezi hayo ambayo yalifwatwa na
wanachama wa chama hicho kuwadhihirishia watanzania kuwa afya yake ni imara
tofauti na inavyozungumzwa na baadhi ya wanasiasa.
Amesema kuwa ni kweli
hapo awali alikuwa anaumwa na alikuwa anasumbuliwa sana na kisukari,na baadae
kukutwa na kansa ya mapafu ambapo amesema kuwa alipata msaada kutoka kwa raisi
JAKAYA KIKWETE akapekwa india na sasa amerejea nchini na madaktari
wamedhibitisha kuwa afya yake ni imara na anaweza kuendelea na mapambano yake
ya kisiasa.
“wale wanaosema kuwa
nina UKIMWI na ninakaribia kufa nawaambia hivi nimepima,na nimekutwa sina huo
ukimwi na namdhihirishia mke wangu kuwa mimi sichepuki,hao wanaosema hivyo
washindwe na wameishiwa kisiasa na watakufa wao waniache,mimi ni mzima na leo
nimetembea toka magomeni hadi hapa bila hata kuweweseka ni ishara kuwa nina
uwezo mkubwa sana bado wakuwaongoza watanzania”alisema waziri huyo wa mambo ya
ndani mstaafu.
Akizungumzia hali ya
kisiasa katika jimbo la vunjo ambalo amekuwa akiliongoza kwa sasa amesema kuwa
kumekuwa na mahasimu wawili ambao wamekuwa wakimnyima usingizi katika jimbo
hilo ambapo amesema kuwa wanamchafua kwa hali na mali kuhakikisha kuwa
wanamwondoa madarakani na kukifuta kabisa chama cha TLP
Hasimu wa kwanza
aliyemtaja ni mbunge wa kuteuliwa ambaye ni mwenyekiti wa chama cha NCCR
mageuzi mh JAMES MBATIA ambapo amesema kuwa kiongozi huyo ametangaza vita ya
wazi wazi na chama chake pamoja na yeye baada ya kuendesha harakati katika jimbo
lake harakati ambazo zilipewa jina la OPERATION DELETE MREMA NA TLP VUNJO,hatua
ambayo mrema anasema kuwa huo sio ufanyaji wa siasa bali ni kuendesha vita ya
chini chini ambayo haina maana.
“mbatia ameanza vita
ambayo ni ya kipumbavu ya kunichafua kuwahonga viongozi wa chama changu ili
wakihasi chama na kujiunga naye,vita ambayo lengo lake ni kuchukua jimbo la
vunjo,sasa mimi nasema hivi hakuna mtu anayeweza kuniondoa vunjo na hatoki mtu
pale”alisema naibu waziri mkuu huyo wa zamani nchini Tanzania.
Aidha amemtaja hasimu
wake mwingine kuwa ni katibu mkuu wa chama cha mapinduzi CCM ndugu ABRAHAN
KINANA ambapo amesema kuwa katibu huyo amekuwa akipita katika jimbo lake
kuwaeleza maneno wanachama wake na wanavunjo maneno ambayo amesema kuwa yana
lengo la kumchafua kisiasa na kumgombanisha na wapiga kura wake.
“hivi kinana ana nini
mbona ananifwata fwata sana kule vunjo,alikuja kule akawaambia wananchi eti
mimi nawaibia hela za mfuko wa jimbo,akasema kuwa zinatoka million 100 kwa
mwaka wakati zinatoka million 42 tu kwa mwaka,amenichafua sana na bahati nzuri
hadi sauti yake ninayo akinichafua na maneno yake na nafwatilia nijue cha
kufanya”alisema mrema
Amesema kuwa
amemwandikia barua Rais kikwete ya kutaka amkanye kinana aache kumfwatilia
katika jimbo lake na pia arudi kule vunjo akakaniushe maneno ambayo aliyatoa
kuwa anawaibia wananchi mara moja kama alivyofanya awali ambapo barua hiyo
tayari imeshamfikia Rais.
Kuhusu chama chake na
jinsi anavyokiendesha amesema kuwa kumekuwa na maneno kuwa anaendesha chama
hicho kama familia yake eti hakina utaratibu amesema kuwa wanaosema hayo maneno
sio watu wazuri kwa chama chake na maisha yake hivyo amewataka wananchi na
watanzania kuendelea kukiamini chama hicho kwani bado ndio jibu la watanzania
kwa sasa.
TLP wapo katika mkutano
mkuu ambao umeanza leo ambao ndani ya mkutano huo pia utafanyika uchaguzi wa
viongozi mbalimbali ndani ya chama hicho.
PICHA ZOTE TOKA MAGOMENI HADI SINZA ZIPO CHINI HAPO
No comments:
Post a Comment